Saturday, 5 June 2021

Vidoda vya tumbo vinakusumbua na hujui nini cha kufanya basi carehelp tunakupa tiba ya tatizo la vidoda vya tumbo.

VIDODA VYA TUMBO.


Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali (tindikali)za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi (tindikali)inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

 

 AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO


Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

       1. Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa

       2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)

 

CHANZO AU SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO


 

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

1 Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)

2 Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)

3 Kuwa na mawazo mengi

4 Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi

5 Kunywa pombe na vinywaji vikali

6 Uvutaji wa sigara

7 Kuto kula mlo kwa mpangilio

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO


 

Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;


1 Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula

2 Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo

3 Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa

4 Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu

5 Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu

6 Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito

7 Kushindwa kupumua vizuri

TIBA.

 

JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO

 

1 Kunywa maji mengi

2 Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo

3 Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)

4 Usivute sigara

5 Punguza au acha kunywa pombe

6 Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali

7 Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

      8    Majani ya fenugreek -chemsha kiasi cha mjani weka na chumvi kidogo kunywa mara mbili kila siku.

      9   Ndizi mbili .Ndizi zinakitu kinaitwa antibacterial substance ambao husaidia kutokua kwa vidoda tumboni kwahiyo kula ndizi moja kila siku baada ya kunywa chai asubuhi.

      10  kabichi mbichi.Tegeneza juisi ya kabichi ni nzuri sana katika kutibu vidoda  fanya kunywa juisi ya kabichi kila siku kabla ya mda wa kulala.

       11  Vitunguu.tafuna kitunguu kimoja au viwili kila siku.

       12  Nazi . Tumia maji ya nazi kunywa kadiri utavyoweza ikiwezekana kila siku itakusaidia kutibu vidoda.


Unaijua bawasiri wewe hivi unahisi ni Maumivu gani mtu anayapitia akipata hili tatizo basi Jifunze zaidi kwa....

BAWASIRI.


Bawasiri (au Kikundu au Futuri au Puru au Mjiko au Hemoroidi kutoka Kiingereza hemorrhoid) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa haja kubwa ambayo husaidia kudhibiti kinyesi, hutenda kazi kama mto uliotengenezwa kwa njia ya vena na tishu unganishi. Huwa patholojia ikiwa hufungana kwa kuvimba au kupata inflamesheni.(uvimbe/Maumivu).

SABABU.

Kisababishi kamili cha hemoroidi hakijulikani.Japo kuna baadhi ya sababu zinazochangia.

  • Ukosefu wa choo (Kufungika kwa chooau kuhara),kwa mda mrefu au kujirudia mara kwa mara.
  • Ukosefu wa mazoezi, 
  • Visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba), 
  • Ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (uchovu unaoendelea kwa muda 
  • Ukubwa wa ndani wa fumbatio, au ujauzito), 
  • Jenetiki, (kurithi)
  • Kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri.
  • Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu,kikohozi kinachoendelea kwa mudana sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.
  • Wakati wa ujauzito, shinikizo kutoka mimbakwa fumbatio na ubadilishaji wa homonihufanya mishipa ya hemoroidi kuwa kubwa. 
  • Kuzaa pia husabibisha ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio.Ni nadra kwa wanawake wajawazito kuhitaji matibabu ya upasuaji, kwa sababu dalili huisha baada ya kuzaa.

DALILI.

Dalili za hemoroidi hulingana na mahali. Hemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa kinyesi kilicho na damu bila maumivu, ilihali hemoroidi za nje zinaweza kutoa dalili chache au ikiwa zina thrombasi maumivu na uvimbe katika sehemu ya haja kubwa. Watu wengi hurejelea kimakosa dalili yoyote inayotokea karibu na sehemu ya rektamu ya hajakubwa . "hemoroidi" na visababishi hatari vya dalili vinapaswa kutupiliwa mbali. Huku kisababishi halisi kikisalia kutojulikana, baadhi ya vipengele vinavyoongeza shinikizo la fumbatio la ndani, hasa kufungika kwa choo, vinaaminika kuchangia ukuaji wa hemoroidi.

TIBA.

  • Matibabu ya mwanzo kula chakula kilicho na faiba, vinywaji ili kudumisha haidresheni, dawa za kutibu inflamesheni husaidia kwa maumivu.
  • Maji ya moto .Tumia maji ya moto weka kwenye beseni na kalia kwa mda wa dakika 10 hadi 15 fanya hivo kutwa mara tatu 
  • Barafu.Tumia kipande cha barafu na weka sehemu ya haja kubwa itakuasaidia kupunguza Maumivu na uvimbe pia .
  • Mazoezi .
  • Muone dakitari kwa uchunguzi zaidi kama hali itazidi kuongezeka 



Tabia ya kukoroma kwa mpenzi wako,Mke/Mme inakukera basi usijari fanya yafuatayo...

KUKOROMA.


 

  •  Kukoroma ni Sauti kali inayotoka puani au mdomoni na hufanyika wakati wa kupumua kukiwa kumezuiliwa kidogo wakati huo ukiwa umelala.
  • tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala na  huwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma wakati asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. 
  • Kukoroma kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji,huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. 
  • Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka.

SABABU.


 

  • Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:


  1. Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.
  2. Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.
  3. Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.
  4. Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.
  5. Umri mkubwa au uzee, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka.
  6. Wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake.
  7. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. 
  8. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. 
  9. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.

DALILI 

  • Utajuaje kama unakoroma au unashida ya kukoroma ukiwa umelala zako usiku 
  • Kukoswa Usigizi.Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo akiwa usingizi pia hukatika 
  • Kuchoka.hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. 
  • Kulegea kwa miguu-hii inakuja mara tu unapoamka unakua na hii hali.
  • Mpenzi,Mme/mke au mtu yeyote wa karibu unaelala nae chumba kimoja au Kitanda kimoja kuweza kukwambia kama unakoroma ukiwa umelala au laa .

TIBA


 

Je utafanya nini ili kutibu hii hali ya kukoroma lakini kubla ya kutibu tatizo hili ni vyema kwanza ujue kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.

2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.

3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.

4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.


Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, jaribu pia yafuatayo:

Punguza uzito

Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.

Wacha kuvuta sigara.

Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.


Pia unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile

  • o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
  • o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
  • o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
  • o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
  • o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.
  • Vilevile fanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofautitofauti  jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo.

                       

VIDODA VYA KINYWA VINASABABISHWA NA NINI NA TIBA JE ....

VIDODA VYA KINYWA 


VIDONDA vya Kinywa ni michubuko inayotokea kwenye mdomo na ulimi. Vidonda hivi husababisha mhusika kupata maumivu kwa maana kinywa ni moja ya sehemu ya mwili yenye mishipa mingi ya fahamu na wakati mwingine vidonda katika kinywa husababisha kushindwa kuongea vizuri,kula,kusukutua meno.

  • Vidonda vya Kinywa hutokea ndani ya mashavu, midomo (lips), ulimi, kingo na kuta za meno pia huweza kusambaa mpaka kwenye koromeo ikiwa havitatibiwa kwa wakati.

Aina za Vidonda vya Kinywa

Vidonda vya mdomo huwa vya duara na hutokea ndani ya kinywa, kwenye ulimi na midomo. Vinaweza kuvimba na kuwa vyeupe, vyekundu au vya kijivu. Inawezekana kuwa na kidonda kimoja au zaidi wakati mmoja na kusambaa ndani ya kinywa.

SABABU 


 

Nini Husababisha Vidonda kwenye Kinywa?

Mara nyingi chanzo cha vidonda kwenye kinywa si cha moja kwa moja. Mara nyingi kidonda kimoja kwenye kinywa husababishwa na uharibifu wa utando laini ndani ya kinywa kwa mfano unapojing’ata kwa bahati mbaya au unapokula chakula kigumu.

Haijulikani wazi ni nini husababisha vidonda kwenye kinywa ambavyo hujirudia mara kwa mara, lakini vitu vinavyochochea ni pamoja na msongo, wasiwasi, mabadiliko ya homoni, mfano, baadhi ya wanawake hupatwa na vidonda mdomoni wanapokuwa kwenye siku zao, ulaji wa baadhi ya vyakula mfano vyenye viungo vingi, kahawa, nyanya na unga wa ngano.

Kutumia dawa ya meno yenye sodium lauryl sulphate na kuacha kuvuta sigara ghafla, wengi wanaoacha kuvuta sigara kwa mara ya kwanza wanaweza kupatwa na vidonda mdomoni.

Vidonda vya Kinywa wakati mwingine husababishwa na magonjwa yanayosababishwa na virusi kama tetekuwanga, magonjwa ya fangasi, magonjwa ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula (Crohn’s Disease, Coeliac Disease), ugonjwa wa kuvimba sehemu za maungio za mwili (Reactive Arthritis), ugonjwa wa kuvimba mishipa ya damu (Behcet’s Disease), kinga ya mwili kudhoofu kutokana na VVU au Lupus, upungufu wa vitamin B na madini chuma.

Pia, Vidonda vya Kinywa vinaweza kusababishwa na matumizi ya dawa mbalimbali kama za kutibu magonjwa mbalimbali mfano kupanda kwa shinikizo la damu na dawa za kutuliza maumivu mfano ibuprofen.

 

DALILI.

  • Maumivu makali kwenye fizi,ulimi 
  • Kuvimba kwa kingo za meno 
  • Kupata homa 
  • Maumivu wakati wa kula,kucheka,kuongea 
  • Kupata shida kusukutua meno vizuri 
  • Kupoteza hamu ya chakula 
  • Kupata Maumivu makali ukila vyakula vyenye chumvi .

TIBA

  • Fanya yafuatayo kuweza kupunguza hatari ya kupata Vidonda vya Kinywa mfano kuepuka vyakula fulani kama vyenye viungo vingi, kahawa au chokoleti.
  • Epuka kula vyakula vya moto au baridi sana ikiwa una vidonda tayari kwa maana huchelewesha kupona kwa vidonda, kula matunda kwa wingi na mboga za majani ili kuongeza vitamin na madini chuma vitu vinavyoongeza kinga ya mwili, kutotafuna vitu vigumu,kusukutua meno yako na mswakij laini, kutumia dawa ya meno isiyo na sodium lauryl sulphate, kupunguza msongo na wasiwasi.
  • Tumia maziwa ya nazi mix na asali kidogo paka sehemu iliyonakidoda.
  • Tumia asali paka sehemu yenye kidoda fanya hivo kila siku mara mbili 
  • Baking soda 🥤tumia pia kupaka sehemu iliyoumia 



KIUNGULIA KINAKUTESA NA HUJUI CHA KUFANYA JIBU HILI HAPA....

KIUNGULIA 


 

  • Kiungulia ni tatizo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ambapo husababishashwa na kucheuliwa kwa mchanganyiko wa tindikali na chakula kutoka tumboni kuelekea katika koo la chakula (eneo kati ya umio na tumbo)mchanganyiko huu wenye tindikali huunguza maeneo hayo na kusababisha maumivu makali katika koo la chakula.
  • Tindikali hii ni salama ikiwa katika tumbo pekee ,sehemu nyingine za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hazina ukuta unaoweza stahimili tindikali hii na moja ya sehemu ya mfumo ambayo hushambuliwa zaidi na tindikali ni sehemu ya koo la chakula Sababu haijaudwa na ukuta sitahimilivu dhidi ya tindikali hii hivyo basi kufika kwa tindikali hii katika koo la chakula husababishwa kuuguzwa kwa eneo na kupelekea maumivu makali kufanana na moto.

SABABU


 

  • Kiungulia husababishwa na vitu vingi lakini kuna sababu kubwa inayopelekea kupata kiungulia ni kutumia vitu ambavyo hupelekea kutegenezwa kwa tindikali nyingi zaidi mwili vitu hivyo ni 
    1. Mahabage 
    2. Viazi 
    3. Mihogo 
    4. Matumizi makubwa ya chumvi chmvi 
    5. Ukosefu wa vyakula venyewe ufumwele 
    6. Matumizi ya pombe na kafeini 
    7. Kitambi kutojihusisha na mazoezi 
    8. Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile dawa za pumu na usingizi .

DALILI

  • Maumivu wakati wa kumeza chakula 
  • Kutapika,kichefuchefu
  • Maumivu ya kifua na tumbo kwenye chemba ya moyo 
  • Muwasho katika koo la chakula 
  • Harufu mbaya ya kinywa 
  • Kushikwa na nimonia 

TIBA

  • Kiungulia kinatibika cha kufanya epuka kutumia vyakula ambavyo husababisha kiungulia kama vile chocolates,soda,na juice 🥤zenye tindikali ,usile chakula kingi kupita kiasi,Epuka kuvaa vitu vinavyobana tumbo baada ya kula,usilale kwa mda wa masaa 2-3mara tu baada ya kula 
  • Siki ya apple cider (apple cider vinegar) chukua maji nusu kikombe chaganya halafu kunywa fanya hivo kila baada ya dakika tano hadi kiungulia kitakapopungua 
  • Lemon 🍋Tegeneza juisi ya limao kunywa hivo hivo bila kichanganya na maji kama utashidwa weka maji kidogo .
  • Baking soda 🥤weka kijiko kimoja cha baking soda weka maji nusu Kikombe cha chai halafu kunywa.
  • Mnanaa-tegeneza mix na maji na kunywa mara tatu kwa siku 
  • Kunywa juisi ya alovera,tumia tangawizi na mbegu za shamari.

NB-kutotibu kiungulia cha mara kwa mara kinaweza pelekea ukapata magonjwa yafuatayo

  • Uvimbe joto sehemu za koo la chakula 
  • Kutegeneza kovu katika koo la chakula 
  • Kubadirika kwa seli za koo na kupelekea koo kushidwa kufanya kazi yake 
  • Saratani ya koo 
  • Vidoda vya tumbo.

Thank you 🙏 

Je?Mgongo,Kiuno kinakutesa umekua ukipata Maumivu ya mara kwa mara basi tiba imepatikana carehelp wanakupa njia nzuri ya kuondoa tatizo lako..

MAUMIVU YA KIUNO,MGONGO NA NYONGA KWA WANAUME NA WANAWAKE.


 

  • Maumivu ya kiuno huamzia chini ya mgongo na kukamata katika vifupa vilivyo chini karibia na makalio.Maumivu haya husambaa kulia na kushoto na wakati mwingine hutelemka hadi mapajani pamoja na kuwepo katika vifupa hivyo pia ndani zaidi huweza kusababisha maumivu kutokea kwa ndani na kusambaa nje katika eneo la kiuno.
  • Maumivu ya nyoga huweza kutokea sambamba na maumivu ya kiuno .Nyonga huunganisha miguu na mifupa ya mapaja inayotegeneza kiuno .Nyonga ndo inakufanya utembee,Inakuwezesha kutoka sehemu moja kwenye sehemu nyingine,Kukaa,kuruka na n.k.

SABABU ZINAZOPELEKEA HAYA MAUMIVU YA KIUNO,NYONGA NA MGONGO


 

  • Kujichua kwa mda mrefu hasa kwa wanaume.
  • Kubeba mizigo mizito kwa kuinama 
  • Namna ya kulala -godoro linaweza pia sababisha maumivu haya 
  • Mawazo -ukiwa na msongo wa mawazo pia unachangia 
  • Kulala kwa mda mrefu na matumizi mabaya ya mto 
  • Ajari -ukipata ajari pia inaweza pelekea ukapata hii shida 
  • Jongo(arthritis) uvimbe maji kwenye magoti 

DALILI ZAKE 

  • Kuhisi homa 
  • Kupungua kwa uzito 
  • Kupata ganzi sehemu ya karibia na haja kubwa
  • Kupata ganzi sehemu za makalio 
  • Kuvimba sehemu ya kiuno 
  • Kushidwa kukojoa au kupata maumivu wakati wa kukojoa 
  • Kuhisi ganzi pia sehemu za siri 
  • Kushidwa au maumivu makali ukiinama 

TIBA

  • Fanya yafuatayo ukiwa nyumbani kama utakua na hii shida kabla ya kwenda kufanya uchunguzi zaidi 
  • Barafu-tumia pakiti ya barafu weka sehemu uliyoumia au unayohisi maumivu ndani ya masaa 24 toka umeanza kuhisi maumivu .
  • Maji ya moto-Tumia maji ya moto kuoga kama maumivu yako yamepitiliza masaa 24 kwani ukitumia barafu zaidi ya masaa 24 toka umeumia hataisaidia 
  • Pata mda mwingi wa kupumzika hasa usiku lala mda wa kutosha kwa usiku na ulale katika sitaili nzuri au utumie mto vizuri.
  • Mazoezi-Ni mhimu pia kufanya mazoezi ya viungo kadiri utakavyoweza Itakusaidia pia kuondokana na maumivu.

NB-maumivuvu ya kiuno ya mda mrefu yanaweza kukupelekea ukapata athari kama.....

  • Kushidwa kufanya tendo la ndoa 
  • Kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili 
  • Kuwahi kufika kileleni mapema wakati wa tendo la ndoa na kushidwa kurudia.
  • Kushidwa Kutembea kunyanyuka