VIDODA VYA KINYWA
VIDONDA vya Kinywa ni michubuko inayotokea kwenye mdomo na ulimi. Vidonda hivi husababisha mhusika kupata maumivu kwa maana kinywa ni moja ya sehemu ya mwili yenye mishipa mingi ya fahamu na wakati mwingine vidonda katika kinywa husababisha kushindwa kuongea vizuri,kula,kusukutua meno.
- Vidonda vya Kinywa hutokea ndani ya mashavu, midomo (lips), ulimi, kingo na kuta za meno pia huweza kusambaa mpaka kwenye koromeo ikiwa havitatibiwa kwa wakati.
Aina za Vidonda vya Kinywa
Vidonda vya mdomo huwa vya duara na hutokea ndani ya kinywa, kwenye ulimi na midomo. Vinaweza kuvimba na kuwa vyeupe, vyekundu au vya kijivu. Inawezekana kuwa na kidonda kimoja au zaidi wakati mmoja na kusambaa ndani ya kinywa.
SABABU
Nini Husababisha Vidonda kwenye Kinywa?
Mara nyingi chanzo cha vidonda kwenye kinywa si cha moja kwa moja. Mara nyingi kidonda kimoja kwenye kinywa husababishwa na uharibifu wa utando laini ndani ya kinywa kwa mfano unapojing’ata kwa bahati mbaya au unapokula chakula kigumu.
Haijulikani wazi ni nini husababisha vidonda kwenye kinywa ambavyo hujirudia mara kwa mara, lakini vitu vinavyochochea ni pamoja na msongo, wasiwasi, mabadiliko ya homoni, mfano, baadhi ya wanawake hupatwa na vidonda mdomoni wanapokuwa kwenye siku zao, ulaji wa baadhi ya vyakula mfano vyenye viungo vingi, kahawa, nyanya na unga wa ngano.
Kutumia dawa ya meno yenye sodium lauryl sulphate na kuacha kuvuta sigara ghafla, wengi wanaoacha kuvuta sigara kwa mara ya kwanza wanaweza kupatwa na vidonda mdomoni.
Vidonda vya Kinywa wakati mwingine husababishwa na magonjwa yanayosababishwa na virusi kama tetekuwanga, magonjwa ya fangasi, magonjwa ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula (Crohn’s Disease, Coeliac Disease), ugonjwa wa kuvimba sehemu za maungio za mwili (Reactive Arthritis), ugonjwa wa kuvimba mishipa ya damu (Behcet’s Disease), kinga ya mwili kudhoofu kutokana na VVU au Lupus, upungufu wa vitamin B na madini chuma.
Pia, Vidonda vya Kinywa vinaweza kusababishwa na matumizi ya dawa mbalimbali kama za kutibu magonjwa mbalimbali mfano kupanda kwa shinikizo la damu na dawa za kutuliza maumivu mfano ibuprofen.
DALILI.
- Maumivu makali kwenye fizi,ulimi
- Kuvimba kwa kingo za meno
- Kupata homa
- Maumivu wakati wa kula,kucheka,kuongea
- Kupata shida kusukutua meno vizuri
- Kupoteza hamu ya chakula
- Kupata Maumivu makali ukila vyakula vyenye chumvi .
TIBA
- Fanya yafuatayo kuweza kupunguza hatari ya kupata Vidonda vya Kinywa mfano kuepuka vyakula fulani kama vyenye viungo vingi, kahawa au chokoleti.
- Epuka kula vyakula vya moto au baridi sana ikiwa una vidonda tayari kwa maana huchelewesha kupona kwa vidonda, kula matunda kwa wingi na mboga za majani ili kuongeza vitamin na madini chuma vitu vinavyoongeza kinga ya mwili, kutotafuna vitu vigumu,kusukutua meno yako na mswakij laini, kutumia dawa ya meno isiyo na sodium lauryl sulphate, kupunguza msongo na wasiwasi.
- Tumia maziwa ya nazi mix na asali kidogo paka sehemu iliyonakidoda.
- Tumia asali paka sehemu yenye kidoda fanya hivo kila siku mara mbili
- Baking soda 🥤tumia pia kupaka sehemu iliyoumia


No comments:
Post a Comment