Sunday, 13 June 2021

KWANINI PUMU NA KWANINI MJAMZITO MWENYE PUMU HUJIFUNGUA MTOT NJITI SABABAU NI .....


ASTHAMA/PUMU 

Pumu ni nini ni ugonjwa unaona athiri sehemu ya mfumo wa hewa kwa maana ya ya bronchial tree kwenda kwenye mapafu.

Bronchial tree ni njia inayotumika kupitisha hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu na kuna njia zaidi ya elfu 1000 kwa kila njia kuu ya bronchial kwa kila pafu.

Pumu hutokea pale kunapokua na mchubuko sugu kwenye njia zake za kupitisha hewa (bronchial tree)amabapo husababisha kuvimba/kujaa kwa mirija hiyo na hua na mucus/ute mzito hali hii hupelekea kushidwa kupita kwa hewa vizuri kuingia ua kutoka kwenye mapafu na kumfanya mhusika apate shida ya kupumua,Na ndo tunaita Pumu au Mtu huyu ana tataizo la Pumu.

Hali hii inaweza kua ya mda mfupi au mda mrefu na ikichukua mda mrefu basi inahitaji tiba ili kuepusha madhara makubwa zaidi kutokea.

AINA ZA PUMU

Pumu imegawanyika katika makundi mawili

  1. Pumu ya ghafra/Acute Asthma - Aina hii ya pumu hua ni ya kawaida na njia zake hua katika hali nzuri na inaweza ikatokea na ikashisha yenyewe ndani ya mda mfupi pasipo kutumia tiba yeyeote.
  2. Pumu Sugu/Chronic Asthma-Aina hii ni tofauti na ile ya kwanza kwani hii njia zake tayari zishakua nyembamba sana kutoka na kuvimba pamoja na kua na ute mwingi mzito hii hutokea pale pumu inapojirudia mara kwa mara na kupelekea kua sugu na tiba huhitajika zaidi ili kua sawa.
SABABU ZA PUMU KUTOKEA.
Vitu vingi sana husababisha au huchangia kutokea kwa Pumu 
  1. Mzio/Allergies. 
  2. Moshi/kuvuta sigara au tumbaku.
  3. Mchafuko wa mazingira/Uchafuzi wa hewa.
  4. Uzito kupita kiasi
  5. Msongo wa mawazo au mawazo 
  6. Kurithi
  7. Maambukizi ya wadudu kwenye mapafu 
  8. Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake.
  9. Baadhi ya vyakula kama samaki,mayai,karanga,na soya
DALILI ZA UGONJWA 
  • Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)
  • Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)
  • Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
  • Kubana kwa kifua.
  • Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.
TIBA YA PUMU
  • Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa (bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia mzio (antihistamine drugs).

Matibabu mengine ni kama ifuatavyo
  • Juisi ya tangawizi chaganya na asali kidogo tumia mbili mara tatu kwa siku.
  • Mafuta ya karatusi masaji sehemu ya kifua hadi utapojisikia nafuu
  • Mafuta ya mikaratusi weka matone kidogo kwenye maji ya moto kiasi na tumia
  • Asali kiasi mix na maji ya moto kiasi na kunywa kutwa mara 2/3
  • Tumia kitunguu,matunda,limao,maziwa na mbegu za shamari.