Tuesday, 15 June 2021

UNAPOTEZA KUMBUKUMBU NA HUJUI KWANINI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI.


FAHAMU UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU (DEMENSHIA)
  • Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Dimenshia)unawapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65 na ni ugonjwa ulio endelevu kwa maana dalili zake huwa zinazidi kuongezeka taratibu kadri siku zinavyozidi kuongezeka.
SABABU YA KUPOTEZA KUMBUKUMBUKU.
  • Visababishi vya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ni nini?
Kupoteza kumbukumbu kunatokea pale Chembechembe za ubongo zinapo kufa na kutofanya kazi sawasawa kama awali na Mara nyingi Mtu ambae tayari ameanza kua na tatizo hili -Dalili za mwanzo ni kua na matatizo katika kumbukumbu za muda mfupi kwa maana ya (short memory). 
Matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo –hii ina maana hewa ya oksijeni kutofika vizuri katika ubongo na mishipa ya damu.
Hii inaweza pia kusababishwa na kiharusi/kupooza kutokana na shinikizo la damu. 
  • Ziko sababu nyingine nyingi kama vile kusinyaa kwa ubongo, Unywaji wa pombe nyingi,UKIMWI nk.
Baadhi ya visababishi hivi vinatibika au kuzuilika.
Hivyo ni muhimu kwenda hospitalini kwa ushauri zaidi.
Watu gani wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wana uwezekano zaidi wa kupata ugonjwa huu

DALILI.
  • Dalili za Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu zinaweza kuwa kama ifuatavyo.
  1. Kusahau mambo mbalimbali mfano njia ya kurudi nyumbani,kusahau watu , kutokumbuka mazungumzo na kurudiarudia maneno.
  2. Mabadiliko katika haiba - Kukosa raha, woga au hasira.
  3. Matatizo katika mawasiliano - Kushindwa kupata maneno sahihi ya kuzungumza au majina sahihi ya vitu.
  4. Katika hatua za mwisho za ugonjwa huu, mgonjwa hushindwa kufanya shughuli za kila siku na anazidi kuwa tegemezi kwa watu wengine.
TIBA.
  • Je ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unatibika?
Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hautibiki ila dalili zaweza kutibiwa
Ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi
Ni muhimu kwa walezi/ndugu kuelewa na dalili na jinsi ya kumsaidia mgonjwa
Je ninaweza kuzuia kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Kula vizuri na kuwa na mfumo bora wa maisha mfano: Kufanya mazoezi mara kwa mara
Kutokula vyakula vya mafuta
Kutovuta sigara na kuepuka ulevi
Kula mlo kamili.
Ni muhimu kwa wazee kujishughulisha na mambo ya kiakili kama vile kusoma
na kujishughulisha na maswala ya kijamii.
Kama una shinikizo la damu au kisukari ni LAZIMA kupata tiba kutoka kwa daktari
 

TATIZO LA KIKWAPA/KUNUKA AU KUTOA HARUFU MBAYA KWAPANI ,SABABU NA TIBA YAKE HII HAPA..

 

KUNUKA KIKWAPA

Kwanini unatoa harufu ya kikwapa

Hili ni tatizo la kutoa harufu isiyo ya kawaida/mbaya sehemu zako za kwapani kwa mwili wa binadamu.

SABABU YA KIKWAPA/KUTOA HARUFU MBAYA KWAPANI.

Tatizo hili husababishwa na bacteria/wadudu wanaovutiwa na jasho au unyevuunyevu chini ya kwapa, hua kero kwako binafisi na hata kwa mtu mwingine aliyeko karibu yako,kwani harufu inayotoka hua ni mbaya na wakati mwingine unaweza ukashidwa kuivumilia

Sababu zingine ni kama ifuatavyo

  • Matatizo ya Figo/Ugonjwa wa figo ukiwa na shida ya figo ni rahisi sana kwako kua na kikwapa.
  • Ini kua na tatizo au shida,
  • Fngasi ukiwa na fangasi pia ni rahisi kua na kikwapa.
  • kwa wenye shida ya sukari/ugonjwa sukari.
DALILI ZA KIKWAPA 
Je! Utajuaje kama unashida ya kikwapa,Hizi hapa ni dalili za mtu mwenye kikwapa/kwapa kutoa harufu mbaya
  • Kuanza kwa kusweti/kutoa jasho jingi mara kwa mara pasivyo kawaida.
  • kusweti/kutoa jasho wakati wa usiku ukiwa umelala pasipo sababu yeyote
  • kuanza kuhisi harufu mbaya mwilini mwako.
Hizi ni baadhi tu ya dalili lakini dalili kuu inajulikana maana kila mtu anajua harufu ya mwili wake ukiona kuna tofauti ya harufu na uliyoizoea basi hapo utakua na kikwapa.

TIBA YA KIKWAPA
Utanya nini ili kuondoa harufu mbaya/kikwapa


  • Usafi-Zingatia usafi wa mwili na usha kwapa kwa maji ya moto kiasi siyo sana
  • Epuka matumizi ya vyakula venye viungo vingi  hasa vitunguu.
  • Nyoa kwapa lako vizuri mara kwa mara .
  • Apply Venegar mara baada ya kumaliza kushave kwapa lako.hii inakusaidia kuzuia au kuua vijidudu vinavyosababia au kupelekea kutoa harufu mbaya ya kwapa
  • Chukua limano kata kipande cha limano na paka kwenye kwapa lako fanya hivo ikiwezekana kila siku au pale unapohisi kuna harufu mbaya inatoka.
  • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya.
  • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.