KUNUKA KIKWAPA
Kwanini unatoa harufu ya kikwapa
Hili ni tatizo la kutoa harufu isiyo ya kawaida/mbaya sehemu zako za kwapani kwa mwili wa binadamu.
SABABU YA KIKWAPA/KUTOA HARUFU MBAYA KWAPANI.
Tatizo hili husababishwa na bacteria/wadudu wanaovutiwa na jasho au unyevuunyevu chini ya kwapa, hua kero kwako binafisi na hata kwa mtu mwingine aliyeko karibu yako,kwani harufu inayotoka hua ni mbaya na wakati mwingine unaweza ukashidwa kuivumilia
Sababu zingine ni kama ifuatavyo- Matatizo ya Figo/Ugonjwa wa figo ukiwa na shida ya figo ni rahisi sana kwako kua na kikwapa.
- Ini kua na tatizo au shida,
- Fngasi ukiwa na fangasi pia ni rahisi kua na kikwapa.
- kwa wenye shida ya sukari/ugonjwa sukari.
DALILI ZA KIKWAPA
Je! Utajuaje kama unashida ya kikwapa,Hizi hapa ni dalili za mtu mwenye kikwapa/kwapa kutoa harufu mbaya
- Kuanza kwa kusweti/kutoa jasho jingi mara kwa mara pasivyo kawaida.
- kusweti/kutoa jasho wakati wa usiku ukiwa umelala pasipo sababu yeyote
- kuanza kuhisi harufu mbaya mwilini mwako.
Hizi ni baadhi tu ya dalili lakini dalili kuu inajulikana maana kila mtu anajua harufu ya mwili wake ukiona kuna tofauti ya harufu na uliyoizoea basi hapo utakua na kikwapa.
TIBA YA KIKWAPA
Utanya nini ili kuondoa harufu mbaya/kikwapa
- Usafi-Zingatia usafi wa mwili na usha kwapa kwa maji ya moto kiasi siyo sana
- Epuka matumizi ya vyakula venye viungo vingi hasa vitunguu.
- Nyoa kwapa lako vizuri mara kwa mara .
- Apply Venegar mara baada ya kumaliza kushave kwapa lako.hii inakusaidia kuzuia au kuua vijidudu vinavyosababia au kupelekea kutoa harufu mbaya ya kwapa
- Chukua limano kata kipande cha limano na paka kwenye kwapa lako fanya hivo ikiwezekana kila siku au pale unapohisi kuna harufu mbaya inatoka.
- Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya.
- Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
- Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.



No comments:
Post a Comment