Friday, 9 July 2021

TIBA YA MBA KWENYE NYWELE SABABU ZAKE PIA....

MBA KWENYE NYWELE

Mba ni tataizo linalowakuta watu wengi hasa wanawake zaidi kuliko wanaume hutokana na seli zilizokufa pale ambapo zinabaki kwa wingi sehemu moja au sehemu tofauti tofauti katika kichwa na kupelekea kutegeneza kama ukurutu kwenye ngozi ya kichwa na kukufanya ukoswe amani au kukudhalilisha kutokana na kuhisi muwasho usio wa kawaida kichwani.

SABABU YA MBA KICHWANI.

Mba husababishwa na vitu vingi lakini katika hali ya kawaidia ngozi ya kichwa ina seli zake na hujimenya yenyewe na kutoa seli zilizozeeka au kuisha mda wake na seli hizi hupotea zenyewe pasipo hata kujua.Ikifikia hatua ya kuonekana basi kuna ongezeko la seli nyingi kwenye ngozi zilizozeeka kutokana na sababu mbalimbali na zikikutana na mafuta ya nywele zinaugana na kutegeneza kama ukurutu au vipande vidogovidogo vyeupe na pale ndo mtu huonekana ana mba na huwatokea zaidi watu wenye mafuta mengi kwenye ngozi zao.

Baadhi ya sababu ni kama ifuatavyo.

  1. Upungufu wa madini ya ziki na vitamini B
  2. Kutokuosha nywele zako mara kwa mara na shapoo
  3. Upungufu wa kinga ya mwili
  4. Msongo wa mawazo .kua katika hali ya mawazo kwa mda mrefu.
  5. Matatizo /magonjwa ya ngozi.
  6. Kutokuchana nywele zako mara kwa mara hasa unafuga nywele au unasuka na unakaa mda mrefu pasipo kufumua au kuzichana.
  7. Ulaji wa vyakula vyenye sukari,mafta na chumvi nyingi na maziwa pia.
  8. Usafi duni wa kuosha nywele zako usha nywele zako mara tatu hadi nne kwa wiki.
  9. Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana hasa jeli ya kulainisha nywele .
  10. Kurithi kutoka kwa wazazi .
  11. Kua na ngozi ya mafuta sana au kavu sana.
  12. Mabadiriko ya homoni 
DALILI ZA MBA
Mara nyingi dalili zake hujulikana kwa kuona au kuhisi 
  1. Kubanduka kwa ngozi huku kukiambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa.
  2. Kua na vipande vidogovidogo vyeupe kwenye ngozi ya kichwa na maeneo ya chini ya mabega au shingo.

  3. Kuhisi una vidoda kichwani
  4. Kubadiriki kwa ngozi ya kichwa kua kavu sana.
  5. Kuhisi kichwa au ngozi ya kichwa kua kavu na kuwasha kwa sana.
TIBA YA MBA 
  1. Mbegu za fenugreek.
    kuchukua vijiko viwili weka kweny maji kiasi acha kwa siku nzima kesho yake kuchukua na paka kwenye ngozi ya kichwa na acha kwa mda wa nusu saa dakika 30 baada ya hapo osha na shapoo fanya hiyvo mara mbili kwa wiki.
  2. Limau .
    Kata kipande cha limau na sugua au paka sehemu ya ngozi au mba na acha kwa mda wa dakika 10 hadi 15 na baada ya hapo osha na maji ya kawaida fanya hivyo mara mbili kwa wiki.

  3. Mafuta ya nazi .
    Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya nazi chaganya na kijiko kimoja cha maji(kamua) ya limau paka kwenye ngozi ya kichwa kwa dakika kadhaa na acha kwa mda wa nusu saa baada ya hapo osha na shapoo fanya hivyo mara mbili kwa wiki.


  4.  

Mwisho zingatia usafi wa kichwa walau mara tatu hadi nne kwa wiki kula mlo wa afya epuka vykula vyenye mafuta mengi,sukari,na chumvi nyingi pia ,Ondoa mawazo n.k na angalia sababu iliyopelekea kua na mba na uachane nayo itakusaidia kwa ushauri zaidi piga/whatsap no.0718662724