Monday, 28 June 2021

JINO/MENO YANAKUMA SABABU,DALILI NA TIBA JE ?...

MAUMIVU YA JINO/MENO

Maumivu ya jino au meno hutokea katikati ya fizi na taya na maumivu hayo yanaweza kua makali kadri mda unavyozidi kuongezeka yanaweza vumilika au yanaweza yasivumilike kuligana na hali yake ikoje na yanaweza tokea kwa wakati fulani na baadae kuisha yenyewe au yanaweza kuwepo kwa mda wote hadi pale utakapotumia dawa za kutuliza maumivu .

SABABU ZA MAUMIVU YA JINO/MENO

Kuna sababu nyingi tofauti tofauti zinapelekea kua na maumivu ya jino au meno na maoja ya sababu hizo ni kama ifuatavyo.

  1. Kuoza kwa meno/jina kutokana na usafi duni wa meno au kinywa .
  2. Ugonjwa wa fizi au matatizo ya taya 
  3. Kuisha kwa ganda la juu linalofunika jino (enamel) jino inakua rahisi kulika na kupasuka pia na kupelekea kusikia maumivu .
  4. Kutafuna vitu vigumu mara kwa mara huchangia pia kwa meno kuharibika 
  5. Kuchokonoa jino au fizi na sitiki(toothpick) au kipande ya mti kwani inakua ni rahisi kuua njia au neva za jino na kuingia maambukizi ya wadudu kupitia hiyo sitiki unayotumia kuchokonoa kipande kilichogandia kwenye jino.
DALILI ZA JINO/MENO KUUMA/MAUMIVU.
Zifuatazo ni dalili unazoweza hisi kama jino lako au meno yako yanatatizo.
  1. Maumivu wakati ya kutafuna kitu chochote .
  2. Uzimbe karibia na fizi au sehemu ya jino linalouma 
  3. Kuhisi homa na maumivu ya kichwa pamoja na taya  sehemu ya jino lenye tatizo.
  4. Meno/jino linakua na ukakasi na kushidwa kuhimili vitu vya baridi au vya moto.
  5. Maumivu au kijisikia vibaya wakati wa kusugua meno na mswaki.

TIBA YA JINO/MENO
Fanya yafuatayo kuzuia njino lako lisiharibike au tibu kama tatayri jino lako linatatizo au una baadhi ya dalili hizo apo juu tumeelezea 
  • Mafuta ya karafuu/Clove oil. weka tone moja au mbili kwenye kijipande cha pamba na paka fizi zako au sehemu iliyonatatizo kutwa mara mbili hadi pale utapojisikia vizuri.
  • Maji ya chumvi/Salt water.Sukutua na maji ya chumvi kiasi na acha kwa sekunde 30 kabla ya kutema unaweza rudia mara mbili au zaidi kadri utavyoweza .
  • Peppermint tea - Chua kijiko kimoja ya aina hii ya majani ya chai weka kwenye nusu kikombe cha maji ya moja acha kwa dakika 20 baadae sukutua na tema au meza unaweza fanya hivo mara kadhaa.
  • Kitunguu saumu/Garlic .Twanga kitunguu saumu weka na chumvi kiasi na weka au paka moja kwa moja sehemu ya jino linayouma itakusaidia kupunguza maumivu na kuondolea ghadhaa 
  • Epuka kula au kunywa kitu chochote ambacho ni cha moto sana au cha baridi sana kama kinafanya maumivu yazidi.
  • Unaweza kutumia nyuzi ya hariri(floss) kusafisha vizuri jino-ondoa vipande vya vyakula vilivyokwama hapo taratibu kwa kupita kila upande wa jino.
  • Kama meno yako yanaukakasi -sugua meno yako kwa kutumia mswaki taratibu kwa dawa ya mswaki 
  • Kuwa na mpango au utartibu mzuri wa usafi wa kinywa chako ili kuzuia meno yako kuoza .