UPARA/KIPARA/BALDNESS/ALOPECIA
Upara ni hali ya kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mara nyingi hukua, hasa kichwani .
Aina ya upara ya kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unaowatokea hatua kwa hatua binadamu wanaume na viumbe hai wengine na ambayo huitwa "mkondo wa upara wa kiume".
Kiasi na mikondo ya upara vinaweza kutofautiana sana, baina ya mikondo ya kiume na ya kike ya alopeshia (androgenic alopecia au alopecia androgenetica), alopecia areata, ambayo huhusisha upotevu wa baadhi ya nywele kichwani na alopecia totalis, ambayo huhusisha upotevu wa nywele zote kichwani, hadi aina iliyokithiri zaidi ambayo ni universalis alopecia, inayohusisha kupoteza nywele zote kichwani na mwilini.
SABABU ZA KUA NA UPARA
- Kurithi
- Mabadiriko ya homoni
- Magonjwa ya ngozi n.k
- Matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kansa,gauti,Msongo wa mawazo, matatizo ya moyo,Presha,Dawa za uzazi wa mpango,matumizi ya dawa za vitamin A kupita kiasi .
- Taratibu utaanza kuhisi nywele mbele ya kichwa zinaanza kupungua.
- Utaanza kuona vijiduara vinajitokeza mbele/nyuma/katika ya kichwa na kuna kua hamna nywele katikati ya hicho kiduara.
- Hatimae nywele ghafra zinaanza kupotea.
- Utaona kama vijikovu vinaongezeka karibia kichwa chote .
- Tengeza juisi ya kitunguu/kisagesage kitunguu na kamua maji yake halafu paka sehemu iliyozulika acha kwa dakika 15 pasipo kuosha.
- Vitunguu visage halafu changanya na mafata kidogo ya nazi chemsha kidogo na viache vipoe baada ya hapo masaji sehemu iliyokua haina nywele.
- Tumia india gooseberry(Amala) weka kijiko kimoja au viwili chaganya na maji ya limao baaada ya hapo masaji sehemu upara ulipo.
- Alovera .paka alovera geli sehemu ya upara
- Yai,chemsha na chukua ile sehemu nyeupe ya yai chaganya na kijiko kimoja cha oliva oil na paka fanya hivo mara kwa mara.


No comments:
Post a Comment