HARUFU MBAYA KINYWANI.
Kutoa harufu mbaya kinywani/mdomoni au kua na harufu mbaya ya kinywa inaweza ikawa kero kwako binafisi au hata kwa watu wanaokuzunguka au mtu wa karibu yako hiili ni tatizo amabalo humpata mtu yeyote katika wakati wowote na mara nyingi hutokea endapo kutakua na usafi hafifu wa kinywa na pengine inaweza kuani chanzo au dalili ya ugonjwa fulani.
SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUA NA HARUFU MBAYA KINYWANI
Kuna vitu vingi amabavyo huchangia au husababisha kua na harufu mbaya ya kinywa ni kama ifuatavyo
- Matumizi ya tumbaku au sigara .
- Usafi wa kinywa kutokuzingatia namna sahihi ya kusafisha kinywa chako.
- Mdomo kua mkavu -Kuna sababu zinazopelekea mdomo kua mkavu mfano mtu wenye ugonjwa wa kisukari
- Dawa baadhi hua na maudhi ya kukufanya utoa harufu mbaya ya kinywa .
- Maambukizi ya kinywa-kua na magonjwa kinywani mfano vidoda au jino kuoza ,
- Saratani na tataizo la kiungulia husababisha pia kutoa harufu mbaya
DALILI ZA KUA NA HARUFU MBAYA KINYWANI
Utajuaje kama unatoa harufu mbaya ya kinywa pengine kwa kijichunguza wewe binafi (toa pumzi kwenye kiganja cha mkono wako halafu ivute hiyo pumzi kwa kutumia mdomo wako au pua) au kwa kuumuliza mtu wako wa karibu kama unavyoongea nae nahisi harufu mbaya yeyote inatoka kinywa kwako
Midomo kua mikavu kila wakati hii pia inaweza kukufanya ujitambue kama unatoa harufu mbya ya kinywa
Radha tamu mdomoni,Kuhisi radha ya tofauti au kubadirika kwa radha mdomoni kwako hii pia itakufanya ujitambue kua harufu ya kinywa chako inayotoka siyo ya kawaida
Mipako kwenye ulimi kama utando utando hii pia ukiona kitu kama hicho kwenye kinywa chako basi tambua kinywa chako hakiko sawa.
TIBA/MATIBABU YA HARUFU MBAYA YA KINYWA.Tiba ni mhimu kwanza kujitambua au kujua harufu mbaya ya kinywa chako imetokana na kitu gani halafu ndo uje kwenye tiba sasa kutibu pekee bila kujua chanzo cha tataizo lako unaweza usipone au ukapona na tataizo likajirundia ndani ya mda mfupi.
Fanya yafuatayo ukiwa nyumbani ili kuondokana na tataizo la harufu mbaya ya kinywa .
- Swaki vizuri kinywa chako kutwa mara tatu unapomaliza kula chakula cha usiku baada ya nusu saa fanya usafi wa kinywa,asubuhi ukiamka pata kwanza kama ni chai au kifungua kinywa baada ya nusu saa ndo uswaki ,mchana ukimaliza kula chakula chako nusu saa badae swaki.Na ukiswaki tema uchafu lakini usisukutue na maji maana kufanya hivo utakua umeondoa kinga yote ambayo iko kwenye dawa yako unayotumia kuswakia kwahiyo ni vyema ukatema uchafu basi au ukasukutua na maji halafu unachukua dawa ya meno unapaka kwenye fizi au kinywa chako.
- Fanya usafi wa ulimi wako kwa kutoa mipako au utando utaojitokeza kwa ulimi wako fanya ivo mara kwa mara kila utapoona kuna kitu kama hicho.
- Kula chakula safi na sahihi kwa afya yako usipende sana kutumia vyakula vyenye sukari nyingi au vinywaji venye sukari mfano pombe,soda,Vyakula venye vitunguu maji na vitunguu swaumu vingi n.k.
- Sukutua mdomo wako na juisi ya limao kutwa mara mbili
- Kunywa chai ya Couple fennel kila siku.

