Tuesday, 15 June 2021

UNAPOTEZA KUMBUKUMBU NA HUJUI KWANINI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI.


FAHAMU UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU (DEMENSHIA)
  • Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Dimenshia)unawapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65 na ni ugonjwa ulio endelevu kwa maana dalili zake huwa zinazidi kuongezeka taratibu kadri siku zinavyozidi kuongezeka.
SABABU YA KUPOTEZA KUMBUKUMBUKU.
  • Visababishi vya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ni nini?
Kupoteza kumbukumbu kunatokea pale Chembechembe za ubongo zinapo kufa na kutofanya kazi sawasawa kama awali na Mara nyingi Mtu ambae tayari ameanza kua na tatizo hili -Dalili za mwanzo ni kua na matatizo katika kumbukumbu za muda mfupi kwa maana ya (short memory). 
Matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo –hii ina maana hewa ya oksijeni kutofika vizuri katika ubongo na mishipa ya damu.
Hii inaweza pia kusababishwa na kiharusi/kupooza kutokana na shinikizo la damu. 
  • Ziko sababu nyingine nyingi kama vile kusinyaa kwa ubongo, Unywaji wa pombe nyingi,UKIMWI nk.
Baadhi ya visababishi hivi vinatibika au kuzuilika.
Hivyo ni muhimu kwenda hospitalini kwa ushauri zaidi.
Watu gani wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wana uwezekano zaidi wa kupata ugonjwa huu

DALILI.
  • Dalili za Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu zinaweza kuwa kama ifuatavyo.
  1. Kusahau mambo mbalimbali mfano njia ya kurudi nyumbani,kusahau watu , kutokumbuka mazungumzo na kurudiarudia maneno.
  2. Mabadiliko katika haiba - Kukosa raha, woga au hasira.
  3. Matatizo katika mawasiliano - Kushindwa kupata maneno sahihi ya kuzungumza au majina sahihi ya vitu.
  4. Katika hatua za mwisho za ugonjwa huu, mgonjwa hushindwa kufanya shughuli za kila siku na anazidi kuwa tegemezi kwa watu wengine.
TIBA.
  • Je ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unatibika?
Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hautibiki ila dalili zaweza kutibiwa
Ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi
Ni muhimu kwa walezi/ndugu kuelewa na dalili na jinsi ya kumsaidia mgonjwa
Je ninaweza kuzuia kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Kula vizuri na kuwa na mfumo bora wa maisha mfano: Kufanya mazoezi mara kwa mara
Kutokula vyakula vya mafuta
Kutovuta sigara na kuepuka ulevi
Kula mlo kamili.
Ni muhimu kwa wazee kujishughulisha na mambo ya kiakili kama vile kusoma
na kujishughulisha na maswala ya kijamii.
Kama una shinikizo la damu au kisukari ni LAZIMA kupata tiba kutoka kwa daktari
 

No comments:

Post a Comment