BAWASIRI.
Bawasiri (au Kikundu au Futuri au Puru au Mjiko au Hemoroidi kutoka Kiingereza hemorrhoid) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa haja kubwa ambayo husaidia kudhibiti kinyesi, hutenda kazi kama mto uliotengenezwa kwa njia ya vena na tishu unganishi. Huwa patholojia ikiwa hufungana kwa kuvimba au kupata inflamesheni.(uvimbe/Maumivu).
SABABU.
Kisababishi kamili cha hemoroidi hakijulikani.Japo kuna baadhi ya sababu zinazochangia.
- Ukosefu wa choo (Kufungika kwa chooau kuhara),kwa mda mrefu au kujirudia mara kwa mara.
- Ukosefu wa mazoezi,
- Visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba),
- Ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (uchovu unaoendelea kwa muda
- Ukubwa wa ndani wa fumbatio, au ujauzito),
- Jenetiki, (kurithi)
- Kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri.
- Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu,kikohozi kinachoendelea kwa mudana sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.
- Wakati wa ujauzito, shinikizo kutoka mimbakwa fumbatio na ubadilishaji wa homonihufanya mishipa ya hemoroidi kuwa kubwa.
- Kuzaa pia husabibisha ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio.Ni nadra kwa wanawake wajawazito kuhitaji matibabu ya upasuaji, kwa sababu dalili huisha baada ya kuzaa.
DALILI.
Dalili za hemoroidi hulingana na mahali. Hemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa kinyesi kilicho na damu bila maumivu, ilihali hemoroidi za nje zinaweza kutoa dalili chache au ikiwa zina thrombasi maumivu na uvimbe katika sehemu ya haja kubwa. Watu wengi hurejelea kimakosa dalili yoyote inayotokea karibu na sehemu ya rektamu ya hajakubwa . "hemoroidi" na visababishi hatari vya dalili vinapaswa kutupiliwa mbali. Huku kisababishi halisi kikisalia kutojulikana, baadhi ya vipengele vinavyoongeza shinikizo la fumbatio la ndani, hasa kufungika kwa choo, vinaaminika kuchangia ukuaji wa hemoroidi.
TIBA.
- Matibabu ya mwanzo kula chakula kilicho na faiba, vinywaji ili kudumisha haidresheni, dawa za kutibu inflamesheni husaidia kwa maumivu.
- Maji ya moto .Tumia maji ya moto weka kwenye beseni na kalia kwa mda wa dakika 10 hadi 15 fanya hivo kutwa mara tatu
- Barafu.Tumia kipande cha barafu na weka sehemu ya haja kubwa itakuasaidia kupunguza Maumivu na uvimbe pia .
- Mazoezi .
- Muone dakitari kwa uchunguzi zaidi kama hali itazidi kuongezeka

Ahsateh kwa elimu
ReplyDelete