Monday, 7 June 2021

U T I IMEKUA SUGU KWAKO NA HUJUI KWANINI UNAPATA U T I MARA KWA MARA.CAREHELP TUNAKUJUZA...


U.T.I/ URINARY TRACK INFECTION 

Ni maambukizi ya bakiteria au wadudu katika njia ya mkojo kwa maana ya kibofu na urethra.


Jinsia ya kike hua na hatari kubwa zaidi ya kupata au kuathrika na U T I  kuliko jinsia ya kiume kwasabau urethra ya mawanamke ni fupi zaidi au iko karibu sana na kibofu cha -mkojo kuliko urethra ya mwanaume yeye iko mbali zaidi kufikia kibofu cha mkojo . 

Maambukizi yakwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea maambukizi yakifika mpaka kwenye figo. 

SABABU YA KUPATA U.T.I



U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.

U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali, tunashauri mtu mwenye U.T.I inatakiwa awe msafi na kubadili mienendo iliyo hatarini.

Kuna aina mbili za U.T.I

  1. Maambukizi ya Upande wa juu – Hii hujumuisha Figo (Pyelonephritis)
  2. Maambukizi ya Upande wa chini – Hii hujumuisha Kibofu (cystitis).

VITU AU CHANZO KINACHOPELEKEA KUPATA U.T.I

vifuatavyo vinaweza kukuingiza kwenye hatari ya kupata U.T.I;

  1. Kinga ya mwili kuto kuwa imara
  2. Kutumia Vifaa au Dawa za kuzuia mimba
  3. Kwa mwanamke; Kupungua kwa homoni ya estrogeni
  4. Mtu mwenye kisukari
  5. Kutumia choo kichafu na kutumia idadi kubwa ya watu
  6. Kuwa na tatizo la mmeng’enyo na tatizo la choo
  7. Kukaa kwa mda mrefu bila kutembeatembea

DALILI ZA MTU MWENYE U.T.IVITU



Dalili za mtu mwenye tatizo la U.T.I hutokea tofauti kulingana na umri, jinsia na sehemu iliyoathiriwa. Hizo dalili ni kama

  1. Kujihisi mchovu na kutokujisikia vizuri
  2. Kukojoa kwa shida na kujilazimisha
  3. Maumivu wakati wa kukojoa
  4. Kukojoa kiasi kidogo cha mkojo na mara kwa mara
  5. Mkojo kutoa harufu kali
  6. Mkojo kuwa na rangi tofauti zisizo za kawaida kwa mfano wekundu kiasi
  7. Kichefuchefu au kutapika
  8. Maumivu ya tumbo, au pande za mwili karibu na tumbo mpaka sehemu za misuli
  9. Joto laweza kuongezeka
  10. Maumivu ya kiuno,nyoga na tumbo chini ya kitovu.

TIBA AU NJISI YA KUEPUKANA NA MAAMBUKIZI YA U T I 

      1. kunywa maji mengi kadiri utavyoweza walau lita 3 kwa siku 

      2. Acha kutumia dawa za uzazi wa mpango

      3. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali

      4. Kojoa hata kidogo baada ya kujamiiana au kushiriki tendo la ndoa 

      5. Punguza au acha kunywa pombe na kutumia sigara huchochea kuathiri kibofu

      6. Kuwa msafi hasa sehemu za siri ili kutoruhusu bakteria

      7. Usipulizie spray kwenye sehemu za siri

      8. Weka matone(drops)10 ya mafata ya miti ya chai kwenye maji yako ya kuoga na Osha seheumu zako za siri na maji hayo.

       9.Kunywa nusu glass ya juis ya cranberry kila siku.

       10. Tumia vitamin C vidoge.

NB.

U.T.I hutibika kwa kuwaondoa bakteria na fangasi sehemu zilizoathirika kwa kutumia dawa, mtu mwenye U.T.I hupata shida sana na mpaka humpelekea kutokuwa na raha. Mtu mwenye U.T.I asipoitibu husababisha vimelea kuzaliana na kuwa vingi hii huitwa U.T.I sugu yuko hatarini kuwa na tatizo kubwa na pia hukaribisha magonjwa mengi.



No comments:

Post a Comment