Tuesday, 13 July 2021

JIFUNZE TIBA YA MAFUA DALILI NA CHANZO CHAKE....

 MAFUA 

 Mafua- Ni aina ya ugonjwa ambao huwakumba watu wengi, na mara nyingi watu wengi husema mafua siyo ugonjwa kwasababu hupatikana kirahisi na inaweza kukutokea mara kwa mara.

Mafua hutokea taratibu na mara kwa mara na yanaweza kua sugu yakiambatana na magonjwa mengine kama nimonia (homa ya mapafu)

SABABU ZINAZOPELEKEA KUA NA MAFUA 

Mafua mara mara nyingi husababishwa na vitu vidogovidogo na yanaweza kuisha yenyewe isipokua kama yamesababishwa na virusi aina ya  rhino virus.

Sababu zinazopelekea kua na mafua ni kama ifuatavyo 

  1. Kungia kwa virusi vya rhino virus kwenye mwili kwa njia ya mdomo na pua.
  2. Kutumia kitambaa/leso(handkerchief)chafu haiko katika hali ya usafi pamoja na taulo(towel)chafu.
  3. Kula mboga mboga mbichi na matunda pasipo kuosha vizuri(chafu).
  4. Kugusana na mtu ambae tayari anafua au virusi ya rhino.
  5. Kunywa maji machafu pamoja na vyakula ambavyo haviko katika mazingira mazuri kwa maana ya uchafu.
DALILI ZA MAFUA 

  1. Maumivu ya kichwa 
  2. Pua kubana,kuwasha au kutokwa na kamasi nyepesi au nzito.
  3. Pua Kuvimba au kua na vidonda kwa ndani.
  4. Kutokwa na machozi ikambatana na macho kuwasha.
  5. Kua na homa
  6. Kua na kikohozi.
  7. Kupiga chafya mara kwa mara.
TIBA 
1. Tumia Limao na Asali.Weka vijiko viwili vya juisi ya limao na vijiko  viwili vya asali changanya na kunywa kutwa mara nne kwa siku.
2. Spice tea
   
 
3.Tangawizi. Kata kipande cha tangawizi na kikate katika vipande vidogovidogo vichemshe na maji kiasi kwa mda wa dakika 3 hadi 4 chuja maji yake weka juisi ya limao na asali kijiko kimoja au viwili changanya na kunywa kutwa mara mbili au mara tatu kwa siku . 


4.Kitunguu maji chemsha au weka kwenye kikombe cha maji ya moto chaganya na kijiko kimoja cha cha Asali  
5.Kitunguu swaumu vipande sita,weka kwenye maji ya moto changanya na juisi tumia mara mbili kwa siku.
 
 
6.Kua mbali na vitu vinavyochangia kua na mafua kama allegiies(Uzio) kama vumbi,maranda ya mbao,uchafu wa nguo,mashuka vumbi la maua n.k

Friday, 9 July 2021

TIBA YA MBA KWENYE NYWELE SABABU ZAKE PIA....

MBA KWENYE NYWELE

Mba ni tataizo linalowakuta watu wengi hasa wanawake zaidi kuliko wanaume hutokana na seli zilizokufa pale ambapo zinabaki kwa wingi sehemu moja au sehemu tofauti tofauti katika kichwa na kupelekea kutegeneza kama ukurutu kwenye ngozi ya kichwa na kukufanya ukoswe amani au kukudhalilisha kutokana na kuhisi muwasho usio wa kawaida kichwani.

SABABU YA MBA KICHWANI.

Mba husababishwa na vitu vingi lakini katika hali ya kawaidia ngozi ya kichwa ina seli zake na hujimenya yenyewe na kutoa seli zilizozeeka au kuisha mda wake na seli hizi hupotea zenyewe pasipo hata kujua.Ikifikia hatua ya kuonekana basi kuna ongezeko la seli nyingi kwenye ngozi zilizozeeka kutokana na sababu mbalimbali na zikikutana na mafuta ya nywele zinaugana na kutegeneza kama ukurutu au vipande vidogovidogo vyeupe na pale ndo mtu huonekana ana mba na huwatokea zaidi watu wenye mafuta mengi kwenye ngozi zao.

Baadhi ya sababu ni kama ifuatavyo.

  1. Upungufu wa madini ya ziki na vitamini B
  2. Kutokuosha nywele zako mara kwa mara na shapoo
  3. Upungufu wa kinga ya mwili
  4. Msongo wa mawazo .kua katika hali ya mawazo kwa mda mrefu.
  5. Matatizo /magonjwa ya ngozi.
  6. Kutokuchana nywele zako mara kwa mara hasa unafuga nywele au unasuka na unakaa mda mrefu pasipo kufumua au kuzichana.
  7. Ulaji wa vyakula vyenye sukari,mafta na chumvi nyingi na maziwa pia.
  8. Usafi duni wa kuosha nywele zako usha nywele zako mara tatu hadi nne kwa wiki.
  9. Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana hasa jeli ya kulainisha nywele .
  10. Kurithi kutoka kwa wazazi .
  11. Kua na ngozi ya mafuta sana au kavu sana.
  12. Mabadiriko ya homoni 
DALILI ZA MBA
Mara nyingi dalili zake hujulikana kwa kuona au kuhisi 
  1. Kubanduka kwa ngozi huku kukiambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa.
  2. Kua na vipande vidogovidogo vyeupe kwenye ngozi ya kichwa na maeneo ya chini ya mabega au shingo.

  3. Kuhisi una vidoda kichwani
  4. Kubadiriki kwa ngozi ya kichwa kua kavu sana.
  5. Kuhisi kichwa au ngozi ya kichwa kua kavu na kuwasha kwa sana.
TIBA YA MBA 
  1. Mbegu za fenugreek.
    kuchukua vijiko viwili weka kweny maji kiasi acha kwa siku nzima kesho yake kuchukua na paka kwenye ngozi ya kichwa na acha kwa mda wa nusu saa dakika 30 baada ya hapo osha na shapoo fanya hiyvo mara mbili kwa wiki.
  2. Limau .
    Kata kipande cha limau na sugua au paka sehemu ya ngozi au mba na acha kwa mda wa dakika 10 hadi 15 na baada ya hapo osha na maji ya kawaida fanya hivyo mara mbili kwa wiki.

  3. Mafuta ya nazi .
    Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya nazi chaganya na kijiko kimoja cha maji(kamua) ya limau paka kwenye ngozi ya kichwa kwa dakika kadhaa na acha kwa mda wa nusu saa baada ya hapo osha na shapoo fanya hivyo mara mbili kwa wiki.


  4.  

Mwisho zingatia usafi wa kichwa walau mara tatu hadi nne kwa wiki kula mlo wa afya epuka vykula vyenye mafuta mengi,sukari,na chumvi nyingi pia ,Ondoa mawazo n.k na angalia sababu iliyopelekea kua na mba na uachane nayo itakusaidia kwa ushauri zaidi piga/whatsap no.0718662724



 

Wednesday, 7 July 2021

TIBA YA KIPANDA USO SABABU NA DALILI ZAKE ZIJUE KWA KUSOMA HAPA...

 

KIPANDA USO 

Kipanda uso Ni maumivu makali ya kichwa upande mmoja ambayo hutokea ghafra kwa mda na yanaweza kuendelea yakiambatana na dalili kwenye macho kushidwa kutazama mwanga vizuri,masikio na mikono pamoja na miguu kukaza.

Kipanda Uso hutokea sana kwa wananaweke sababu huonekana kurithiwi zaidi kutoka kwenye familia zao kupitia jeni zilizo kwenye chembechembe za damu zao.

SABABU ZA KUTOKEA KWA KIPANDA USO 

Kipanda uso mara nyingi sababau zake hazijulikani haswa ni nini zaidi kinasababisha ingawa kuna hizi sababu huchangia zaidi kwa kiasi kikubwa kutokea kwa kipanda uso .

  1. Uvutaji wa sigara au kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine anaevuta sigara .
  2. Mabadiriko ya mfumo wa homoni kwa wanawake .
  3. Mawazo,Mvutano/hasira,Hofu /wasiwasi,Msongo wa mawazo,
  4. Kutazama kitu chenye mwanga mkali kama Tv,Laptop,Simu kwa mda mrefu,Kua sehemu yenye kelele nyingi,Kua kwenye chumba chenye moshi mwingi,Joto kali,Kuvuta harufu mbaya/kali kwa mda au manukato makali/harufu kali.
  5. Kutokupata mda mzuri wa kulala(Kulala kidogo au sana).
  6. Matumizi ya dawa za usingizi pamoja na uzazi wa mpango
  7. Aleji/Uzio.
  8. Chakula kilichochacha au kusindikwa au chumvi nyingi huweza kuamsha kipanda uso pamoja na kufunga au kutokula kwa wakati.
  9. Jeraha kichwani
  10. Baridi kali kama barafu.
  11. Kutofanya mazoezi 
  12. Kunywa wine nyekundu.
DALILI ZA KIPANDA USO .
  1. Aura( Kubadirika kwa mfumo wa fahamu kama vile kuona unamulikwa na mwanga mkali wakati hakuna mwanga na kuhisi umeguswa mwilini wakati hujaguswa)
  2. Kujihisi kua na msongo wa mawazo wakati huo ukiwa na kipanda uso.
  3. Kushidwa kulala vizuri na kwa wakati.
  4. Kukoswa choo au kukosa choo/haja kubwa 
  5. Maumivu kidogo kidogo au sana upande mmoja wa kichwa .
  6. Kushidwa kugeuza shingo upande mwingine(neck stiffness)
  7. Kichefu chefu pamoja na kutapika.
  8. Mumivu makali ya kichwa upande au pande zote na yanaweza pelekea ukapoteza fahamu,Kichwa kupwitapwita.
  9. Kutokwa na kamasi na macho kutoa machozi kutokana na maumivu makali.
  10. Macho au mishipa ya macho pamoja na shingo kupata maumivu.
  11. Kua na hali ya kubanwa na mkojo au kukojoa mara kiwa mara .
  12. Kupata maumivu makali zaidi unapokua kwenye mwanga.
  13. Kufifia kwa vitu vinavyokuzunguka pamoja na kizunguzungu.
TIBA YA KIPANDA USO.
  • Tangawizi.

    Kunywa chai yenye tangawizi nyingi ya kutosha  mara kadhaa hadi pale maumivu yatakapopungua .
  • Kifurushi cha barafu.

    Weka kipacho cha barafu nyuma ya shingo yako kwa mda wa dakika kadhaa hadi utapohisi maumivu yamepoa.
  • Apple Cider vinegar.

    Chukua kijiko kimoja chaganya na asali kijiko kimoja weka kwenye glasi ya maji na kunywa kila siku.
  • Pilipili ya cayenne.


    Kata kipande kidogo cha pilipili au kiasi kidogo cha uga wa pilipili ya cayenne weka kwenye kikombe cha maji ya moto weka na maji ya limao na asali changanya na kunywa kila siku .
  • Chamomile tea.

    Kunywa chai yenye majani haya weka maji ya limao na asali  na kunywa mara 3 hadi 4 kwa siku.
N.B Hizi ni aina ya vyakula ambavyo vinaweza sababisha kipanda uso.
  1. Vinywaji vyenye sukari isiyo asili kama juis kola n.k
  2. Vinywaji venye kafeini.
  3. Matunda aina ya citrus kama machungwa na ndimu n.k.
  4. Vyakula vyenye kemikali aina ya tyramine kama cheese zilizokaa mda mrefu
  5. Nyama yenye kemikali ya nitrates.
Mwisho tiba pia kutokana na sababu iliyopelekea kua na kipanda uso kwa mawasiliano au ushauri zaidi piga/whatsap 0718662724.

Monday, 5 July 2021

JE UNAKITAMBI AU TUMBO KUBWA NA UGEPENDA KUJUA NAMNA YA KUONDOA SOMA...

KITAMBI 

Ni Murundikano wa mafuta kwenye tumbo na yanaweza kua chini ya ngozi au ndani kabisa kuzunguka tumbo.Mafuta ya ndani ya tumbo yanaweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kaiasi gani,mafuta haya huhitajika mwilini kwa ajiri ya kuteganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusunguana lakini yakizidi huleta madhara makubwa kama magonjwa ya sukari,presha ,magonjwa ya moyo ,kansa ya maziwa na kansa ya utumbo  Vilevile kukupotezea muonekana muzuri wa umbo lako.

SABABU ZINAZOPELEKEA KUA NA TUMBO KUBWA AU KITAMBI 

Sababu za kua na kitambi zipo nyingi sana na hii hutokea pale kunapokosekana ulingano mzuri wa kalori mwilini kutokana na kula vyakula vyenye kalori nyingi sana kuliko njisi amabavyo utaweza kutumia na kutoa kama taka mwili. Sababu ni kama ifuatavyo

  1. Kula vyakula vingi vyenye kalori(Nguvu)kuliko matumizi yake.
  2. Kula vyakula vingi vya wanga kama vile ugali wa mahindi,mihogo,wali,viazi vya mviringo na ndizi pia kila siku au mara kwa mara..
  3. Msongo wa mawazo -Kua na murundikano wa mawazo kunaweza haribu ufanisi wa kumenganya chakula kwa wakati na kupelekea kua na kitambi.
  4. Kubadirika kwa homone.
  5. Matumizi ya vyakula feki (junk food) kama vile vinywaji vyenye sukari nyingi,pizza,baga,juisi za matunda,chipis,maandazi ,chapati na vitu vingine vya kukaanga n.k.
  6. Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kulala.
  7. Kukaa mda mwingi kwenye kiti.
  8. Matumizi ya Nyama mara kwa mara hata kama ni ya kuchemsha,kukaanga au kuchoma.
  9. Kurithi kutoka kwa wazazi .
  10. Kutojishughulisha na mazoezi.
  11. Maisha ya kuiga kama ulevi wa pombe na kadharika.
DALILI ZA KUA NA KITAMBI AU TUMBO KUBWA 
  1. Tumbo kua kubwa na kubana ukivaa nguo
  2. Uchovu  

TIBA AU NJISI YA KUONDOA KITAMBI/TUMBO KUBWA 
  • Kunywa maji mengi kwa siku walau lita tatu au zaidi na dakika 15 baada ya kumaliza kula au kabla ya kula 
  • Kunywa Green tea kila siku 
  • Kula spicy foods vyakula vyenye viungo
  • Weka nazi katika chakula chako 
  • Tafuna nyanya moja au mbili kila siku 
  • Tangawizi -twanga kipande cha tangawizi kamua maji yake weka na asali kidogo subiri kwa dakika tano na kunywa kila siku .
  • Kunywa juis/maji ya limao kila siku 
  • Tafuna  kitunguu swaumu vipande vitatu au vinne asubuhi  na baada ya hapo kunywa maji ya limao kila siku.
  • Kula mlo mzuri wenye protein matunda na mbogamboga na kuacha vyakula vya waga na junks foods vyakula feki
  • Fanaya mazoezi walau dakika 30 kwa kila siku.
  • Epukana na mawazo.
Kwa ushauri zaidi piga/whatsaap 0718662724.

Thursday, 1 July 2021

JIFUNZE KUHUSU P . I .D/MAAMBUKIZI YA WADUDU KWENYE VIA VYA UZAZI, DALILI ZAKE SABABU NA TIBA PIA


P.I.D/MAAMBUKIZI YA WADUDU KWENYE VIA VYA UZAZI,
P.I.D- Pelvic Inflammatory Disease.
P.I.D Ni maambukizi kwenye via vya uzazi kwa mwanamke ambayo huusisha maambukizi kwenye shingo ya kizazi(CERVICITIS),nyama kwenye mfumo wa wa uzazi(ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi(SALPINGITIS) 
Kuna aina mbili ambayo ni chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa P.I.D ni NEISSERIA GONORNOAE na CHLAMYDIA TRACHOMATIC

WANAMKE ANAUPATAJE UGONJWA WA P.I.D 
-Kupitia ngono zembe
-Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
-Kufanya mapenzi bila kutumia kinga
-Kupitia magonjwa ya zinaa hususani kaswande na kisonono
-Kupitia kunyonywa ukeni mara kwa mara
-Utoaji wa mimba na kutosafishwa vizuri baada ya kutoa mimba
-Kuweka vitu ukeni ili kuufanye uke ubane au kumvutia mpenzi wako
-Kutumia dawa na njia za kuzuia mimba(vijiti na sindano)
- Kuwa na U.T.I. sugu au fungus ya muda mrefu
-Kupitia kufanya mapenzi kinyume na maumbile (haja kubwa)kwa mwanamke.

DALILI ZA P.I.D
-Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri yaweza ukawa njano, mweupe au maziwa
-Uke kutoa harufu mbaya 
-Kuwashwa sehemu za siri
-Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
-Uke kuwa mlaini sana
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa
-Kuvurugika kwa hedhi
-Kutokwa na maji maji ukeni kupita kiasi
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Homa, uchovu na kizunguzungu

MADHARA YA P.I.D 
-Maumivu ya tumbo au nyonga ya mara kwa mara mara baada ya tendo la ndoa. au kipindi cha upevushaji mayai hali hii hutokana na majeraha yaliyopi katika mirija ya uzazi
-Kusababisha majeraha ndani na nje ya mirija za uzazi ambayo hipelekea mirija kuziba
-Kubeba mimba nje ya kizazi husababishwa yai kushindwa kufika kwenywe mji wa uzazi kupitia mirija ya uzazi 
-Ugumba kwa mwanamke
-kupata kansa ya shingo ya uzazi 

JINSI YA KUEPUKANA NA P.I.D
Japo kuwepo na tiba za kujitibu lakini unashauriwa kinga ni bore kuliko tiba hivyo zingatia yafuatayo;-
-Epuka kufanya ngono zembe
-Usifanye mapenzi baada ya kujifungua au mimba kutoka
-Weka tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara
-Kuwa msafi na nguo zako za ndani na kula lishe bora
-Epuka kushare nguo za ndani
-Usifanye mapenzi kinyume na maumbile kupitia haja kubwa,kunyonywa sehemu za siri n.k

UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA HUU WAHI KUPATA MATIBABU. KWANI UGONJWA HUU NI HATARI NA HUWEZA KUKUSABABISHIA UGUMBA AU KANSA YA SHINGO YA KIZAZI

N.B 
Ugonjwa wa P.I.D unatibika vizuri kabisa hivy basi kama upo tayari unaumwa piga namba hii ili kuweza kupata tiba piga/whatsap 0718662724.

Monday, 28 June 2021

JINO/MENO YANAKUMA SABABU,DALILI NA TIBA JE ?...

MAUMIVU YA JINO/MENO

Maumivu ya jino au meno hutokea katikati ya fizi na taya na maumivu hayo yanaweza kua makali kadri mda unavyozidi kuongezeka yanaweza vumilika au yanaweza yasivumilike kuligana na hali yake ikoje na yanaweza tokea kwa wakati fulani na baadae kuisha yenyewe au yanaweza kuwepo kwa mda wote hadi pale utakapotumia dawa za kutuliza maumivu .

SABABU ZA MAUMIVU YA JINO/MENO

Kuna sababu nyingi tofauti tofauti zinapelekea kua na maumivu ya jino au meno na maoja ya sababu hizo ni kama ifuatavyo.

  1. Kuoza kwa meno/jina kutokana na usafi duni wa meno au kinywa .
  2. Ugonjwa wa fizi au matatizo ya taya 
  3. Kuisha kwa ganda la juu linalofunika jino (enamel) jino inakua rahisi kulika na kupasuka pia na kupelekea kusikia maumivu .
  4. Kutafuna vitu vigumu mara kwa mara huchangia pia kwa meno kuharibika 
  5. Kuchokonoa jino au fizi na sitiki(toothpick) au kipande ya mti kwani inakua ni rahisi kuua njia au neva za jino na kuingia maambukizi ya wadudu kupitia hiyo sitiki unayotumia kuchokonoa kipande kilichogandia kwenye jino.
DALILI ZA JINO/MENO KUUMA/MAUMIVU.
Zifuatazo ni dalili unazoweza hisi kama jino lako au meno yako yanatatizo.
  1. Maumivu wakati ya kutafuna kitu chochote .
  2. Uzimbe karibia na fizi au sehemu ya jino linalouma 
  3. Kuhisi homa na maumivu ya kichwa pamoja na taya  sehemu ya jino lenye tatizo.
  4. Meno/jino linakua na ukakasi na kushidwa kuhimili vitu vya baridi au vya moto.
  5. Maumivu au kijisikia vibaya wakati wa kusugua meno na mswaki.

TIBA YA JINO/MENO
Fanya yafuatayo kuzuia njino lako lisiharibike au tibu kama tatayri jino lako linatatizo au una baadhi ya dalili hizo apo juu tumeelezea 
  • Mafuta ya karafuu/Clove oil. weka tone moja au mbili kwenye kijipande cha pamba na paka fizi zako au sehemu iliyonatatizo kutwa mara mbili hadi pale utapojisikia vizuri.
  • Maji ya chumvi/Salt water.Sukutua na maji ya chumvi kiasi na acha kwa sekunde 30 kabla ya kutema unaweza rudia mara mbili au zaidi kadri utavyoweza .
  • Peppermint tea - Chua kijiko kimoja ya aina hii ya majani ya chai weka kwenye nusu kikombe cha maji ya moja acha kwa dakika 20 baadae sukutua na tema au meza unaweza fanya hivo mara kadhaa.
  • Kitunguu saumu/Garlic .Twanga kitunguu saumu weka na chumvi kiasi na weka au paka moja kwa moja sehemu ya jino linayouma itakusaidia kupunguza maumivu na kuondolea ghadhaa 
  • Epuka kula au kunywa kitu chochote ambacho ni cha moto sana au cha baridi sana kama kinafanya maumivu yazidi.
  • Unaweza kutumia nyuzi ya hariri(floss) kusafisha vizuri jino-ondoa vipande vya vyakula vilivyokwama hapo taratibu kwa kupita kila upande wa jino.
  • Kama meno yako yanaukakasi -sugua meno yako kwa kutumia mswaki taratibu kwa dawa ya mswaki 
  • Kuwa na mpango au utartibu mzuri wa usafi wa kinywa chako ili kuzuia meno yako kuoza .

Wednesday, 23 June 2021

TIBA YA HARUFU MBAYA YA KINYWA/MDOMONI....

 HARUFU MBAYA KINYWANI.

Kutoa harufu mbaya kinywani/mdomoni au kua na harufu mbaya ya kinywa  inaweza ikawa kero kwako binafisi au hata kwa watu wanaokuzunguka au mtu wa karibu yako hiili ni tatizo amabalo humpata mtu yeyote katika wakati wowote na mara nyingi hutokea endapo kutakua na usafi hafifu wa kinywa na pengine inaweza kuani chanzo au dalili ya ugonjwa fulani.

SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUA NA HARUFU MBAYA KINYWANI

Kuna vitu vingi amabavyo huchangia au husababisha kua na harufu mbaya ya kinywa ni kama ifuatavyo

  1. Matumizi ya tumbaku au sigara .
  2. Usafi wa kinywa kutokuzingatia namna sahihi ya kusafisha kinywa chako.
  3. Mdomo kua mkavu -Kuna sababu zinazopelekea mdomo kua mkavu mfano mtu wenye ugonjwa wa kisukari 
  4. Dawa baadhi hua na maudhi ya kukufanya utoa harufu mbaya ya kinywa .
  5. Maambukizi ya kinywa-kua na magonjwa kinywani mfano vidoda au jino kuoza ,
  6. Saratani na tataizo la kiungulia husababisha pia kutoa harufu mbaya

 DALILI ZA KUA NA HARUFU MBAYA KINYWANI

Utajuaje kama unatoa harufu mbaya ya kinywa pengine kwa kijichunguza wewe binafi (toa pumzi kwenye kiganja cha mkono wako halafu ivute hiyo pumzi kwa kutumia mdomo wako au pua) au kwa kuumuliza mtu wako wa karibu kama unavyoongea nae nahisi harufu mbaya yeyote inatoka kinywa kwako

Midomo kua mikavu kila wakati hii pia inaweza kukufanya ujitambue kama unatoa harufu mbya ya kinywa

Radha tamu mdomoni,Kuhisi radha ya tofauti au kubadirika kwa radha mdomoni kwako hii pia itakufanya ujitambue kua harufu ya kinywa chako inayotoka siyo ya kawaida 

Mipako kwenye ulimi kama utando utando hii pia ukiona kitu kama hicho kwenye kinywa chako basi tambua kinywa chako hakiko sawa.

TIBA/MATIBABU YA HARUFU MBAYA YA KINYWA.

Tiba ni mhimu kwanza kujitambua au kujua harufu mbaya ya kinywa chako imetokana na kitu gani halafu ndo uje kwenye tiba sasa kutibu pekee bila kujua chanzo cha tataizo lako unaweza usipone au ukapona na tataizo likajirundia ndani ya mda mfupi.

Fanya yafuatayo ukiwa nyumbani ili kuondokana na tataizo la harufu mbaya ya kinywa .

  1. Swaki vizuri kinywa chako kutwa mara tatu unapomaliza kula chakula cha usiku baada ya nusu saa fanya usafi wa kinywa,asubuhi ukiamka pata kwanza kama ni chai au kifungua kinywa baada ya nusu saa ndo uswaki ,mchana ukimaliza kula chakula chako nusu saa badae swaki.Na ukiswaki tema uchafu lakini usisukutue na maji maana kufanya hivo utakua umeondoa kinga yote ambayo iko kwenye dawa yako unayotumia kuswakia kwahiyo ni vyema ukatema uchafu basi au ukasukutua na maji halafu unachukua dawa ya meno unapaka kwenye fizi au kinywa chako.
  2. Fanya usafi wa ulimi wako kwa kutoa mipako au utando utaojitokeza kwa ulimi wako fanya ivo mara kwa mara kila utapoona kuna kitu kama hicho.
  3. Kula chakula safi na sahihi kwa afya yako usipende sana kutumia vyakula vyenye sukari nyingi au vinywaji venye sukari mfano pombe,soda,Vyakula venye vitunguu maji na vitunguu swaumu vingi n.k.
  4. Sukutua mdomo wako na juisi ya limao kutwa mara mbili
  5. Kunywa chai ya Couple fennel kila siku.
N.B Ukifanya yote haya na bado kuna harufu mbaya ya kinywa inaendelea ni vyema ukamuona dakitari kwa ushauri zaidi.

Monday, 21 June 2021

MZIO/ALEJI HUTOKANA NA KITU GANI NA TIBA YAKE JE!......

MZIO/ALEJI/ALLERGIES.

Mzio - Ni Muuitiko wa kinga ya mwili usio kawaida ambapo hutokea pale kinga ya mwili inapopambana na kitu kingine amabacho kimeingia mwilini kwa njia yeyote ile mfano kumeza,kupaka,kuvuta,kugusana au kugusa kitu na hupelekea kutokea kwa aleji au mzio.

Kutokea kwa hali hii kati ya kinga ya mwili na kitu kingine ambacho kimeingia mwilini kwa njia yeyote ile huwa hakileti madhara.

SABABU YA MZIO/ALEJI/ALLERGIES

Ni kitu gani au nini kinasababisha kwa mtu kua na mzio au kutokewa na aleji,Kuna vitu vingi au sababu nyingi zinazopelekea au kuchangia kutokea kwa mpambano wa kinga ya mwili na kitu kingine ambacho kimeingia mwilini kwa njia yeyote ile na kwa kawaida Mfumo wa kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu hatarishi kama bakteria na virusi.Mfumo huu hupambana na kitu chochote kigeni kinachoingia mwilini.

  1. Mzio wa hewa/Vumbi.
  2. Baadhi ya vyakula 
  3. Kuumwa na wadudu
  4. Baadhi nya dawa/Madawa.
  5. Mpira au baadhi ya vitu unavyovishika.
DALILI YA MZIO/ALEJI/ALLERGIES.
Kuna aina nyingi za mzio au aleji na aina hizi hugawanywa kulingna na vitu vinavyosababisha au mahali unapotokea Mfano mzio unaosababishwa na hewa/vumbi,manyoya ya wanyama ,madawa,chakula au nyasi kavu,amazio kwenye ngozi ,pua au macho.
Zifuatazo ni dalili za Mzio.
  1. Ngozi kua na vipele au mabaka.
  2. Kichwa kuumwa 
  3. Kuwashwa kwenye pua,mdomo,koo,ngozi,au maeneo mengine.
  4. Kuhara
  5. matatizo ya kupumua (kukohoa,kupumua kwa shida)
  6. Kutokwa machozi na kuwashwa kwa macho
  7. Macho kuvimba na kuwa mekundu
  8. Tumbo kuuma 
  9. Kutapika.
  10. Kutiririkwa kwa makamasi.
  11. Kichefuchefu.
TIBA/MATIBABU YA MZIO/ALEJI.
  • Peppermint tea.Tumia aina hii ya majani chukua maji ya moto weka kiasi kidogo cha peppermint tea na subiri kwa dakika 3 had 5 baada ya hapo vuta mvuke wenye hiyo harufu ya chai yenye pepermint na unaweza ukanywa pia ikipoa .
  • Asali.Tumia kijiko kimoja cha asali au zaidi lakini usitumie nyingi zaidi kwa siku.
  • Chukua kitunguu cha rangi nyekundu  kikatekate kisha weka kwenye maji kwa mda kadhaa 1 -2 hrs baada ya hapo kunywa maji yake kila siku.
    Hizi ni tiba unazoweza kuzitumia pasipo kutumia dawa na kama itashindikana basi utahitaji kumuona dakitari kwa uchunguzi zaidi .Lakini pia unaweza angalia chazo au sababu ya mzio umesababishwa na kitu gani mfano chakula au kitu kingine na ukajaribu kukikiacha kwa mda ili kuweza kuona kama aleji yako pengine imesababishwa na hicho kitu.

NB.Mzio/Aleji ya tataizo la kurithi lakini kama wazazi wako wote wawili wana mzio kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na tatizo hili.Uwezekano wa kua na mzio ni mkubwa zaidi kama mama anao pia.Tatizo hili linaweza kufanya aina flani ya magaonjwa kuwa mbaya zaidi kwa mfano pumu na ukurutu.  

Thursday, 17 June 2021

UPARA/KIPARA NINI CHANZO CHAKE NA TIBA JE!.............


UPARA/KIPARA/BALDNESS/ALOPECIA

Upara ni hali ya kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mara nyingi hukua, hasa kichwani .

Aina ya upara ya kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unaowatokea hatua kwa hatua binadamu wanaume na viumbe hai wengine na ambayo huitwa "mkondo wa upara wa kiume".

Kiasi na mikondo ya upara vinaweza kutofautiana sana, baina ya mikondo ya kiume na ya kike ya alopeshia (androgenic alopecia au alopecia androgenetica), alopecia areata, ambayo huhusisha upotevu wa baadhi ya nywele kichwani na alopecia totalis, ambayo huhusisha upotevu wa nywele zote kichwani, hadi aina iliyokithiri zaidi ambayo ni universalis alopecia, inayohusisha kupoteza nywele zote kichwani na mwilini. 

SABABU ZA KUA NA UPARA 

  1. Kurithi
  2. Mabadiriko ya homoni 
  3. Magonjwa ya ngozi n.k
  4. Matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kansa,gauti,Msongo wa mawazo, matatizo ya moyo,Presha,Dawa za uzazi wa mpango,matumizi ya dawa za vitamin A kupita kiasi .
DALILI ZA UPARA
  1. Taratibu utaanza kuhisi nywele mbele ya kichwa zinaanza kupungua.
  2. Utaanza kuona vijiduara vinajitokeza mbele/nyuma/katika ya kichwa na kuna kua hamna nywele katikati ya hicho kiduara.
  3. Hatimae nywele ghafra zinaanza kupotea.
  4. Utaona kama vijikovu vinaongezeka karibia kichwa chote .
TIBA YA UPARA /KIPARA
  •  Tengeza juisi ya kitunguu/kisagesage kitunguu na kamua maji yake halafu paka sehemu iliyozulika acha kwa dakika 15 pasipo kuosha.
  • Vitunguu visage halafu changanya na mafata kidogo ya nazi chemsha kidogo na viache vipoe baada ya hapo masaji sehemu iliyokua haina nywele.
  • Tumia india gooseberry(Amala) weka kijiko kimoja au viwili chaganya na maji ya limao baaada ya hapo masaji sehemu upara ulipo.
  • Alovera .paka alovera geli sehemu ya upara 
  • Yai,chemsha na chukua ile sehemu nyeupe ya yai chaganya na kijiko kimoja cha oliva oil na paka fanya hivo mara kwa mara.
NB- Tumia njia moja wapo au mbili au tatu kutibu tatizo lako la upara/kipara na angalia sababu iliyopelekea kua na kipara/upara.

Tuesday, 15 June 2021

UNAPOTEZA KUMBUKUMBU NA HUJUI KWANINI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI.


FAHAMU UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU (DEMENSHIA)
  • Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Dimenshia)unawapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65 na ni ugonjwa ulio endelevu kwa maana dalili zake huwa zinazidi kuongezeka taratibu kadri siku zinavyozidi kuongezeka.
SABABU YA KUPOTEZA KUMBUKUMBUKU.
  • Visababishi vya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ni nini?
Kupoteza kumbukumbu kunatokea pale Chembechembe za ubongo zinapo kufa na kutofanya kazi sawasawa kama awali na Mara nyingi Mtu ambae tayari ameanza kua na tatizo hili -Dalili za mwanzo ni kua na matatizo katika kumbukumbu za muda mfupi kwa maana ya (short memory). 
Matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo –hii ina maana hewa ya oksijeni kutofika vizuri katika ubongo na mishipa ya damu.
Hii inaweza pia kusababishwa na kiharusi/kupooza kutokana na shinikizo la damu. 
  • Ziko sababu nyingine nyingi kama vile kusinyaa kwa ubongo, Unywaji wa pombe nyingi,UKIMWI nk.
Baadhi ya visababishi hivi vinatibika au kuzuilika.
Hivyo ni muhimu kwenda hospitalini kwa ushauri zaidi.
Watu gani wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wana uwezekano zaidi wa kupata ugonjwa huu

DALILI.
  • Dalili za Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu zinaweza kuwa kama ifuatavyo.
  1. Kusahau mambo mbalimbali mfano njia ya kurudi nyumbani,kusahau watu , kutokumbuka mazungumzo na kurudiarudia maneno.
  2. Mabadiliko katika haiba - Kukosa raha, woga au hasira.
  3. Matatizo katika mawasiliano - Kushindwa kupata maneno sahihi ya kuzungumza au majina sahihi ya vitu.
  4. Katika hatua za mwisho za ugonjwa huu, mgonjwa hushindwa kufanya shughuli za kila siku na anazidi kuwa tegemezi kwa watu wengine.
TIBA.
  • Je ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unatibika?
Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hautibiki ila dalili zaweza kutibiwa
Ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi
Ni muhimu kwa walezi/ndugu kuelewa na dalili na jinsi ya kumsaidia mgonjwa
Je ninaweza kuzuia kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu?
Kula vizuri na kuwa na mfumo bora wa maisha mfano: Kufanya mazoezi mara kwa mara
Kutokula vyakula vya mafuta
Kutovuta sigara na kuepuka ulevi
Kula mlo kamili.
Ni muhimu kwa wazee kujishughulisha na mambo ya kiakili kama vile kusoma
na kujishughulisha na maswala ya kijamii.
Kama una shinikizo la damu au kisukari ni LAZIMA kupata tiba kutoka kwa daktari
 

TATIZO LA KIKWAPA/KUNUKA AU KUTOA HARUFU MBAYA KWAPANI ,SABABU NA TIBA YAKE HII HAPA..

 

KUNUKA KIKWAPA

Kwanini unatoa harufu ya kikwapa

Hili ni tatizo la kutoa harufu isiyo ya kawaida/mbaya sehemu zako za kwapani kwa mwili wa binadamu.

SABABU YA KIKWAPA/KUTOA HARUFU MBAYA KWAPANI.

Tatizo hili husababishwa na bacteria/wadudu wanaovutiwa na jasho au unyevuunyevu chini ya kwapa, hua kero kwako binafisi na hata kwa mtu mwingine aliyeko karibu yako,kwani harufu inayotoka hua ni mbaya na wakati mwingine unaweza ukashidwa kuivumilia

Sababu zingine ni kama ifuatavyo

  • Matatizo ya Figo/Ugonjwa wa figo ukiwa na shida ya figo ni rahisi sana kwako kua na kikwapa.
  • Ini kua na tatizo au shida,
  • Fngasi ukiwa na fangasi pia ni rahisi kua na kikwapa.
  • kwa wenye shida ya sukari/ugonjwa sukari.
DALILI ZA KIKWAPA 
Je! Utajuaje kama unashida ya kikwapa,Hizi hapa ni dalili za mtu mwenye kikwapa/kwapa kutoa harufu mbaya
  • Kuanza kwa kusweti/kutoa jasho jingi mara kwa mara pasivyo kawaida.
  • kusweti/kutoa jasho wakati wa usiku ukiwa umelala pasipo sababu yeyote
  • kuanza kuhisi harufu mbaya mwilini mwako.
Hizi ni baadhi tu ya dalili lakini dalili kuu inajulikana maana kila mtu anajua harufu ya mwili wake ukiona kuna tofauti ya harufu na uliyoizoea basi hapo utakua na kikwapa.

TIBA YA KIKWAPA
Utanya nini ili kuondoa harufu mbaya/kikwapa


  • Usafi-Zingatia usafi wa mwili na usha kwapa kwa maji ya moto kiasi siyo sana
  • Epuka matumizi ya vyakula venye viungo vingi  hasa vitunguu.
  • Nyoa kwapa lako vizuri mara kwa mara .
  • Apply Venegar mara baada ya kumaliza kushave kwapa lako.hii inakusaidia kuzuia au kuua vijidudu vinavyosababia au kupelekea kutoa harufu mbaya ya kwapa
  • Chukua limano kata kipande cha limano na paka kwenye kwapa lako fanya hivo ikiwezekana kila siku au pale unapohisi kuna harufu mbaya inatoka.
  • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya.
  • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.


Sunday, 13 June 2021

KWANINI PUMU NA KWANINI MJAMZITO MWENYE PUMU HUJIFUNGUA MTOT NJITI SABABAU NI .....


ASTHAMA/PUMU 

Pumu ni nini ni ugonjwa unaona athiri sehemu ya mfumo wa hewa kwa maana ya ya bronchial tree kwenda kwenye mapafu.

Bronchial tree ni njia inayotumika kupitisha hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu na kuna njia zaidi ya elfu 1000 kwa kila njia kuu ya bronchial kwa kila pafu.

Pumu hutokea pale kunapokua na mchubuko sugu kwenye njia zake za kupitisha hewa (bronchial tree)amabapo husababisha kuvimba/kujaa kwa mirija hiyo na hua na mucus/ute mzito hali hii hupelekea kushidwa kupita kwa hewa vizuri kuingia ua kutoka kwenye mapafu na kumfanya mhusika apate shida ya kupumua,Na ndo tunaita Pumu au Mtu huyu ana tataizo la Pumu.

Hali hii inaweza kua ya mda mfupi au mda mrefu na ikichukua mda mrefu basi inahitaji tiba ili kuepusha madhara makubwa zaidi kutokea.

AINA ZA PUMU

Pumu imegawanyika katika makundi mawili

  1. Pumu ya ghafra/Acute Asthma - Aina hii ya pumu hua ni ya kawaida na njia zake hua katika hali nzuri na inaweza ikatokea na ikashisha yenyewe ndani ya mda mfupi pasipo kutumia tiba yeyeote.
  2. Pumu Sugu/Chronic Asthma-Aina hii ni tofauti na ile ya kwanza kwani hii njia zake tayari zishakua nyembamba sana kutoka na kuvimba pamoja na kua na ute mwingi mzito hii hutokea pale pumu inapojirudia mara kwa mara na kupelekea kua sugu na tiba huhitajika zaidi ili kua sawa.
SABABU ZA PUMU KUTOKEA.
Vitu vingi sana husababisha au huchangia kutokea kwa Pumu 
  1. Mzio/Allergies. 
  2. Moshi/kuvuta sigara au tumbaku.
  3. Mchafuko wa mazingira/Uchafuzi wa hewa.
  4. Uzito kupita kiasi
  5. Msongo wa mawazo au mawazo 
  6. Kurithi
  7. Maambukizi ya wadudu kwenye mapafu 
  8. Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake.
  9. Baadhi ya vyakula kama samaki,mayai,karanga,na soya
DALILI ZA UGONJWA 
  • Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)
  • Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)
  • Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
  • Kubana kwa kifua.
  • Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.
TIBA YA PUMU
  • Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa (bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia mzio (antihistamine drugs).

Matibabu mengine ni kama ifuatavyo
  • Juisi ya tangawizi chaganya na asali kidogo tumia mbili mara tatu kwa siku.
  • Mafuta ya karatusi masaji sehemu ya kifua hadi utapojisikia nafuu
  • Mafuta ya mikaratusi weka matone kidogo kwenye maji ya moto kiasi na tumia
  • Asali kiasi mix na maji ya moto kiasi na kunywa kutwa mara 2/3
  • Tumia kitunguu,matunda,limao,maziwa na mbegu za shamari. 

Friday, 11 June 2021

CHANZO CHA KWIKWI NA MATIBABU YAKE.

 

HICCUP/KWIKWI

Kwikwi-Ni Ile hali ya kubanwa ghafla na pumzi zinazotoka kinywani kwa nguvu na kwa sauti ya kushitukiza shitukiza wakati usioutegemea kutokana na kushituka na kusinyaa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji kwa maana ya diaphram ambapo hali hii hujurudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu pasipo kawaida au kwa kifupi tunasema ni kutokua na maelewano kati ya diaphram(Misuli ya upumuaji) na mapafu(Lungs).

Kwihiyo hali hii inapotokea kwa milango mikuu ya upumuaji kutokua katika hali yake ya kawaida hupelekea kusikika sauti isiyokua ya kawaida na huita Kwikwi.

SABABU ZA KUPATA KWIKWI.

Hizi sababu za kwikwi ya mda mfupi.

  1. Kua na kikohozi cha mda mrefu
  2. Kuvuta hewa nyingi kupita kiasi kwa mara moja
  3. Kula haraka haraka/kula sana kupita kiasi 
  4. Kucheka sana.
  5. Kupata Uoga wa ghafla wa kitu flani
  6. Kunywa pombe nyingi kwa mpigo
  7. Kua na upungufu wa maji mwilini
  8. Kua na gesi au tumbo kujaa gesi
  9. Kula huku unaongeaongea.