Wednesday, 7 July 2021

TIBA YA KIPANDA USO SABABU NA DALILI ZAKE ZIJUE KWA KUSOMA HAPA...

 

KIPANDA USO 

Kipanda uso Ni maumivu makali ya kichwa upande mmoja ambayo hutokea ghafra kwa mda na yanaweza kuendelea yakiambatana na dalili kwenye macho kushidwa kutazama mwanga vizuri,masikio na mikono pamoja na miguu kukaza.

Kipanda Uso hutokea sana kwa wananaweke sababu huonekana kurithiwi zaidi kutoka kwenye familia zao kupitia jeni zilizo kwenye chembechembe za damu zao.

SABABU ZA KUTOKEA KWA KIPANDA USO 

Kipanda uso mara nyingi sababau zake hazijulikani haswa ni nini zaidi kinasababisha ingawa kuna hizi sababu huchangia zaidi kwa kiasi kikubwa kutokea kwa kipanda uso .

  1. Uvutaji wa sigara au kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine anaevuta sigara .
  2. Mabadiriko ya mfumo wa homoni kwa wanawake .
  3. Mawazo,Mvutano/hasira,Hofu /wasiwasi,Msongo wa mawazo,
  4. Kutazama kitu chenye mwanga mkali kama Tv,Laptop,Simu kwa mda mrefu,Kua sehemu yenye kelele nyingi,Kua kwenye chumba chenye moshi mwingi,Joto kali,Kuvuta harufu mbaya/kali kwa mda au manukato makali/harufu kali.
  5. Kutokupata mda mzuri wa kulala(Kulala kidogo au sana).
  6. Matumizi ya dawa za usingizi pamoja na uzazi wa mpango
  7. Aleji/Uzio.
  8. Chakula kilichochacha au kusindikwa au chumvi nyingi huweza kuamsha kipanda uso pamoja na kufunga au kutokula kwa wakati.
  9. Jeraha kichwani
  10. Baridi kali kama barafu.
  11. Kutofanya mazoezi 
  12. Kunywa wine nyekundu.
DALILI ZA KIPANDA USO .
  1. Aura( Kubadirika kwa mfumo wa fahamu kama vile kuona unamulikwa na mwanga mkali wakati hakuna mwanga na kuhisi umeguswa mwilini wakati hujaguswa)
  2. Kujihisi kua na msongo wa mawazo wakati huo ukiwa na kipanda uso.
  3. Kushidwa kulala vizuri na kwa wakati.
  4. Kukoswa choo au kukosa choo/haja kubwa 
  5. Maumivu kidogo kidogo au sana upande mmoja wa kichwa .
  6. Kushidwa kugeuza shingo upande mwingine(neck stiffness)
  7. Kichefu chefu pamoja na kutapika.
  8. Mumivu makali ya kichwa upande au pande zote na yanaweza pelekea ukapoteza fahamu,Kichwa kupwitapwita.
  9. Kutokwa na kamasi na macho kutoa machozi kutokana na maumivu makali.
  10. Macho au mishipa ya macho pamoja na shingo kupata maumivu.
  11. Kua na hali ya kubanwa na mkojo au kukojoa mara kiwa mara .
  12. Kupata maumivu makali zaidi unapokua kwenye mwanga.
  13. Kufifia kwa vitu vinavyokuzunguka pamoja na kizunguzungu.
TIBA YA KIPANDA USO.
  • Tangawizi.

    Kunywa chai yenye tangawizi nyingi ya kutosha  mara kadhaa hadi pale maumivu yatakapopungua .
  • Kifurushi cha barafu.

    Weka kipacho cha barafu nyuma ya shingo yako kwa mda wa dakika kadhaa hadi utapohisi maumivu yamepoa.
  • Apple Cider vinegar.

    Chukua kijiko kimoja chaganya na asali kijiko kimoja weka kwenye glasi ya maji na kunywa kila siku.
  • Pilipili ya cayenne.


    Kata kipande kidogo cha pilipili au kiasi kidogo cha uga wa pilipili ya cayenne weka kwenye kikombe cha maji ya moto weka na maji ya limao na asali changanya na kunywa kila siku .
  • Chamomile tea.

    Kunywa chai yenye majani haya weka maji ya limao na asali  na kunywa mara 3 hadi 4 kwa siku.
N.B Hizi ni aina ya vyakula ambavyo vinaweza sababisha kipanda uso.
  1. Vinywaji vyenye sukari isiyo asili kama juis kola n.k
  2. Vinywaji venye kafeini.
  3. Matunda aina ya citrus kama machungwa na ndimu n.k.
  4. Vyakula vyenye kemikali aina ya tyramine kama cheese zilizokaa mda mrefu
  5. Nyama yenye kemikali ya nitrates.
Mwisho tiba pia kutokana na sababu iliyopelekea kua na kipanda uso kwa mawasiliano au ushauri zaidi piga/whatsap 0718662724.

No comments:

Post a Comment