Mishipa ya vena(varicose veins) Ni ugonjwa wa kuvimba au kuongezeka ukubwa wa vena kwa maana ya mishapa damu hii hutokea mara baada tu ya mishipa ya damu pamoja na valvu zinazoruhusu damu kusafiri upande mmoja kuharibika au kwenda katika njia isiyo sahihi na hivyo kuifanya damu ijikusanye katika mishipa, Na Pindi inapojikusanya inakuwa nyingi na kupelekea mishipa itanuke zaidi na kufanya ionekane kama mizizi katika usawa wa ngozi,hua katika muonekano wa rangi ya bluu au `zambarau nyeusi.
Varicose veins hutokea sehemu yeyote ya mwili japo mara nyingi hupendelea sana sehemu zilizowazi au zinazoonekana mfano miguuni,nyuma ya paja n.k
1. Umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelea .
2. Ujauzito, kutokana na kuongezeka kwa homones nyingi vile vile kasi ya msukumo wa damu huongezeka na kupelekea vena kuongezeka ukubwa .
3. Hali ya kua na tabia ya kusimama mda mrefu pasipo kukaa-Hii hupelekea presha kubwa zaidi katika miguu na kufanya valvu na mishapa ya damu kuharibika na kusababisha varicose vein kutokea.
4. Uzito,kua na uzito mkubwa kupita kiasi huchangia kwa vena kuongezeka.
5. Shida ya choo/Constipation hii hutokea pale unapokua na shida ya kupata choo kawaida na kujituta unatumia nguvu kubwa zaidi kujisaidia- nguvu unayoitumia inaweza pelekea mishapa ya damu kutanuka zaidi na kusababisha varicose veins.
6. Kurithi kutoka katika familia au ukoo wako.(upande wa mama au upande wa baba)
DALILI ZA VARICOSE VEINS
Dalili za varicose veins mara nyingi ziko wazi maana zinaonekana hata kwa macho mfano wa hizo dalili ni kama ifuatavyo.
1. Muonekano wa vena hua na rangi ya bluu au zambarau nyeusi.
2. Kuhisi maumivu, kuwasha katika sehemu yenye tatizo.
3. Kuvimba kwa miguu na kubadilika kwa muonekano wa miguu yako.mfano huonekana kama mizizi katika usawa wa ngozi.
4. Mishapa ya vena kutoa damu.
TIBA YA VARICOSE VEINS
Kama uko na shida hii fanya yafuatayo itakusaidia kuondokana na shida ya vena .
1. Weka kijiko kimoja cha pipili ya cayenne ambayo iko katika mfumo wa unga katika nusu kikombe cha maji ya moto changanya halafu kunywa kutwa mara tatu kwa siku.
2. Kula vyakula aina ya samaki ,matunda kwa wingi aina tofauti tofauti(siyo juisi ya matunda) na tumia mbogamboga kwa wingi.
3. Usitumie vyakula vyenye sukari nyingi,Ice cream,vyakula vya kukaanga, karanga,vyakula visivyo na taka,jibini,tumbaku,chumvi nyingi,pombe,vyama.
4. Nguo za kubana-kwa wale mnaopenda nguo za kubana ni hatari kwani zinaweza kupelekea ukapata tataizo la varicose veins sa jitaidi kuepuka kuvaa aina hii ya mavazi.
5. Mazoezi,jitaidi kufanya mazoezi kadiri utavyoweza.
6. Vaa soksi ndefu miguu za kubana.
7. Epuka kusimama/kukaa mda mrefu zaidi.
Nb -Kua na varicose veins kuweza kua kumesababishwa na tatizo la kublock kwa mishapa ya damu (Deep Vein thrombosis- DVT) ni vyema ukamuona dakitari za uchunguzi zaidi.



No comments:
Post a Comment