Tuesday, 13 July 2021

JIFUNZE TIBA YA MAFUA DALILI NA CHANZO CHAKE....

 MAFUA 

 Mafua- Ni aina ya ugonjwa ambao huwakumba watu wengi, na mara nyingi watu wengi husema mafua siyo ugonjwa kwasababu hupatikana kirahisi na inaweza kukutokea mara kwa mara.

Mafua hutokea taratibu na mara kwa mara na yanaweza kua sugu yakiambatana na magonjwa mengine kama nimonia (homa ya mapafu)

SABABU ZINAZOPELEKEA KUA NA MAFUA 

Mafua mara mara nyingi husababishwa na vitu vidogovidogo na yanaweza kuisha yenyewe isipokua kama yamesababishwa na virusi aina ya  rhino virus.

Sababu zinazopelekea kua na mafua ni kama ifuatavyo 

  1. Kungia kwa virusi vya rhino virus kwenye mwili kwa njia ya mdomo na pua.
  2. Kutumia kitambaa/leso(handkerchief)chafu haiko katika hali ya usafi pamoja na taulo(towel)chafu.
  3. Kula mboga mboga mbichi na matunda pasipo kuosha vizuri(chafu).
  4. Kugusana na mtu ambae tayari anafua au virusi ya rhino.
  5. Kunywa maji machafu pamoja na vyakula ambavyo haviko katika mazingira mazuri kwa maana ya uchafu.
DALILI ZA MAFUA 

  1. Maumivu ya kichwa 
  2. Pua kubana,kuwasha au kutokwa na kamasi nyepesi au nzito.
  3. Pua Kuvimba au kua na vidonda kwa ndani.
  4. Kutokwa na machozi ikambatana na macho kuwasha.
  5. Kua na homa
  6. Kua na kikohozi.
  7. Kupiga chafya mara kwa mara.
TIBA 
1. Tumia Limao na Asali.Weka vijiko viwili vya juisi ya limao na vijiko  viwili vya asali changanya na kunywa kutwa mara nne kwa siku.
2. Spice tea
   
 
3.Tangawizi. Kata kipande cha tangawizi na kikate katika vipande vidogovidogo vichemshe na maji kiasi kwa mda wa dakika 3 hadi 4 chuja maji yake weka juisi ya limao na asali kijiko kimoja au viwili changanya na kunywa kutwa mara mbili au mara tatu kwa siku . 


4.Kitunguu maji chemsha au weka kwenye kikombe cha maji ya moto chaganya na kijiko kimoja cha cha Asali  
5.Kitunguu swaumu vipande sita,weka kwenye maji ya moto changanya na juisi tumia mara mbili kwa siku.
 
 
6.Kua mbali na vitu vinavyochangia kua na mafua kama allegiies(Uzio) kama vumbi,maranda ya mbao,uchafu wa nguo,mashuka vumbi la maua n.k

Friday, 9 July 2021

TIBA YA MBA KWENYE NYWELE SABABU ZAKE PIA....

MBA KWENYE NYWELE

Mba ni tataizo linalowakuta watu wengi hasa wanawake zaidi kuliko wanaume hutokana na seli zilizokufa pale ambapo zinabaki kwa wingi sehemu moja au sehemu tofauti tofauti katika kichwa na kupelekea kutegeneza kama ukurutu kwenye ngozi ya kichwa na kukufanya ukoswe amani au kukudhalilisha kutokana na kuhisi muwasho usio wa kawaida kichwani.

SABABU YA MBA KICHWANI.

Mba husababishwa na vitu vingi lakini katika hali ya kawaidia ngozi ya kichwa ina seli zake na hujimenya yenyewe na kutoa seli zilizozeeka au kuisha mda wake na seli hizi hupotea zenyewe pasipo hata kujua.Ikifikia hatua ya kuonekana basi kuna ongezeko la seli nyingi kwenye ngozi zilizozeeka kutokana na sababu mbalimbali na zikikutana na mafuta ya nywele zinaugana na kutegeneza kama ukurutu au vipande vidogovidogo vyeupe na pale ndo mtu huonekana ana mba na huwatokea zaidi watu wenye mafuta mengi kwenye ngozi zao.

Baadhi ya sababu ni kama ifuatavyo.

  1. Upungufu wa madini ya ziki na vitamini B
  2. Kutokuosha nywele zako mara kwa mara na shapoo
  3. Upungufu wa kinga ya mwili
  4. Msongo wa mawazo .kua katika hali ya mawazo kwa mda mrefu.
  5. Matatizo /magonjwa ya ngozi.
  6. Kutokuchana nywele zako mara kwa mara hasa unafuga nywele au unasuka na unakaa mda mrefu pasipo kufumua au kuzichana.
  7. Ulaji wa vyakula vyenye sukari,mafta na chumvi nyingi na maziwa pia.
  8. Usafi duni wa kuosha nywele zako usha nywele zako mara tatu hadi nne kwa wiki.
  9. Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana hasa jeli ya kulainisha nywele .
  10. Kurithi kutoka kwa wazazi .
  11. Kua na ngozi ya mafuta sana au kavu sana.
  12. Mabadiriko ya homoni 
DALILI ZA MBA
Mara nyingi dalili zake hujulikana kwa kuona au kuhisi 
  1. Kubanduka kwa ngozi huku kukiambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa.
  2. Kua na vipande vidogovidogo vyeupe kwenye ngozi ya kichwa na maeneo ya chini ya mabega au shingo.

  3. Kuhisi una vidoda kichwani
  4. Kubadiriki kwa ngozi ya kichwa kua kavu sana.
  5. Kuhisi kichwa au ngozi ya kichwa kua kavu na kuwasha kwa sana.
TIBA YA MBA 
  1. Mbegu za fenugreek.
    kuchukua vijiko viwili weka kweny maji kiasi acha kwa siku nzima kesho yake kuchukua na paka kwenye ngozi ya kichwa na acha kwa mda wa nusu saa dakika 30 baada ya hapo osha na shapoo fanya hiyvo mara mbili kwa wiki.
  2. Limau .
    Kata kipande cha limau na sugua au paka sehemu ya ngozi au mba na acha kwa mda wa dakika 10 hadi 15 na baada ya hapo osha na maji ya kawaida fanya hivyo mara mbili kwa wiki.

  3. Mafuta ya nazi .
    Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya nazi chaganya na kijiko kimoja cha maji(kamua) ya limau paka kwenye ngozi ya kichwa kwa dakika kadhaa na acha kwa mda wa nusu saa baada ya hapo osha na shapoo fanya hivyo mara mbili kwa wiki.


  4.  

Mwisho zingatia usafi wa kichwa walau mara tatu hadi nne kwa wiki kula mlo wa afya epuka vykula vyenye mafuta mengi,sukari,na chumvi nyingi pia ,Ondoa mawazo n.k na angalia sababu iliyopelekea kua na mba na uachane nayo itakusaidia kwa ushauri zaidi piga/whatsap no.0718662724



 

Wednesday, 7 July 2021

TIBA YA KIPANDA USO SABABU NA DALILI ZAKE ZIJUE KWA KUSOMA HAPA...

 

KIPANDA USO 

Kipanda uso Ni maumivu makali ya kichwa upande mmoja ambayo hutokea ghafra kwa mda na yanaweza kuendelea yakiambatana na dalili kwenye macho kushidwa kutazama mwanga vizuri,masikio na mikono pamoja na miguu kukaza.

Kipanda Uso hutokea sana kwa wananaweke sababu huonekana kurithiwi zaidi kutoka kwenye familia zao kupitia jeni zilizo kwenye chembechembe za damu zao.

SABABU ZA KUTOKEA KWA KIPANDA USO 

Kipanda uso mara nyingi sababau zake hazijulikani haswa ni nini zaidi kinasababisha ingawa kuna hizi sababu huchangia zaidi kwa kiasi kikubwa kutokea kwa kipanda uso .

  1. Uvutaji wa sigara au kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine anaevuta sigara .
  2. Mabadiriko ya mfumo wa homoni kwa wanawake .
  3. Mawazo,Mvutano/hasira,Hofu /wasiwasi,Msongo wa mawazo,
  4. Kutazama kitu chenye mwanga mkali kama Tv,Laptop,Simu kwa mda mrefu,Kua sehemu yenye kelele nyingi,Kua kwenye chumba chenye moshi mwingi,Joto kali,Kuvuta harufu mbaya/kali kwa mda au manukato makali/harufu kali.
  5. Kutokupata mda mzuri wa kulala(Kulala kidogo au sana).
  6. Matumizi ya dawa za usingizi pamoja na uzazi wa mpango
  7. Aleji/Uzio.
  8. Chakula kilichochacha au kusindikwa au chumvi nyingi huweza kuamsha kipanda uso pamoja na kufunga au kutokula kwa wakati.
  9. Jeraha kichwani
  10. Baridi kali kama barafu.
  11. Kutofanya mazoezi 
  12. Kunywa wine nyekundu.
DALILI ZA KIPANDA USO .
  1. Aura( Kubadirika kwa mfumo wa fahamu kama vile kuona unamulikwa na mwanga mkali wakati hakuna mwanga na kuhisi umeguswa mwilini wakati hujaguswa)
  2. Kujihisi kua na msongo wa mawazo wakati huo ukiwa na kipanda uso.
  3. Kushidwa kulala vizuri na kwa wakati.
  4. Kukoswa choo au kukosa choo/haja kubwa 
  5. Maumivu kidogo kidogo au sana upande mmoja wa kichwa .
  6. Kushidwa kugeuza shingo upande mwingine(neck stiffness)
  7. Kichefu chefu pamoja na kutapika.
  8. Mumivu makali ya kichwa upande au pande zote na yanaweza pelekea ukapoteza fahamu,Kichwa kupwitapwita.
  9. Kutokwa na kamasi na macho kutoa machozi kutokana na maumivu makali.
  10. Macho au mishipa ya macho pamoja na shingo kupata maumivu.
  11. Kua na hali ya kubanwa na mkojo au kukojoa mara kiwa mara .
  12. Kupata maumivu makali zaidi unapokua kwenye mwanga.
  13. Kufifia kwa vitu vinavyokuzunguka pamoja na kizunguzungu.
TIBA YA KIPANDA USO.
  • Tangawizi.

    Kunywa chai yenye tangawizi nyingi ya kutosha  mara kadhaa hadi pale maumivu yatakapopungua .
  • Kifurushi cha barafu.

    Weka kipacho cha barafu nyuma ya shingo yako kwa mda wa dakika kadhaa hadi utapohisi maumivu yamepoa.
  • Apple Cider vinegar.

    Chukua kijiko kimoja chaganya na asali kijiko kimoja weka kwenye glasi ya maji na kunywa kila siku.
  • Pilipili ya cayenne.


    Kata kipande kidogo cha pilipili au kiasi kidogo cha uga wa pilipili ya cayenne weka kwenye kikombe cha maji ya moto weka na maji ya limao na asali changanya na kunywa kila siku .
  • Chamomile tea.

    Kunywa chai yenye majani haya weka maji ya limao na asali  na kunywa mara 3 hadi 4 kwa siku.
N.B Hizi ni aina ya vyakula ambavyo vinaweza sababisha kipanda uso.
  1. Vinywaji vyenye sukari isiyo asili kama juis kola n.k
  2. Vinywaji venye kafeini.
  3. Matunda aina ya citrus kama machungwa na ndimu n.k.
  4. Vyakula vyenye kemikali aina ya tyramine kama cheese zilizokaa mda mrefu
  5. Nyama yenye kemikali ya nitrates.
Mwisho tiba pia kutokana na sababu iliyopelekea kua na kipanda uso kwa mawasiliano au ushauri zaidi piga/whatsap 0718662724.

Monday, 5 July 2021

JE UNAKITAMBI AU TUMBO KUBWA NA UGEPENDA KUJUA NAMNA YA KUONDOA SOMA...

KITAMBI 

Ni Murundikano wa mafuta kwenye tumbo na yanaweza kua chini ya ngozi au ndani kabisa kuzunguka tumbo.Mafuta ya ndani ya tumbo yanaweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kaiasi gani,mafuta haya huhitajika mwilini kwa ajiri ya kuteganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusunguana lakini yakizidi huleta madhara makubwa kama magonjwa ya sukari,presha ,magonjwa ya moyo ,kansa ya maziwa na kansa ya utumbo  Vilevile kukupotezea muonekana muzuri wa umbo lako.

SABABU ZINAZOPELEKEA KUA NA TUMBO KUBWA AU KITAMBI 

Sababu za kua na kitambi zipo nyingi sana na hii hutokea pale kunapokosekana ulingano mzuri wa kalori mwilini kutokana na kula vyakula vyenye kalori nyingi sana kuliko njisi amabavyo utaweza kutumia na kutoa kama taka mwili. Sababu ni kama ifuatavyo

  1. Kula vyakula vingi vyenye kalori(Nguvu)kuliko matumizi yake.
  2. Kula vyakula vingi vya wanga kama vile ugali wa mahindi,mihogo,wali,viazi vya mviringo na ndizi pia kila siku au mara kwa mara..
  3. Msongo wa mawazo -Kua na murundikano wa mawazo kunaweza haribu ufanisi wa kumenganya chakula kwa wakati na kupelekea kua na kitambi.
  4. Kubadirika kwa homone.
  5. Matumizi ya vyakula feki (junk food) kama vile vinywaji vyenye sukari nyingi,pizza,baga,juisi za matunda,chipis,maandazi ,chapati na vitu vingine vya kukaanga n.k.
  6. Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kulala.
  7. Kukaa mda mwingi kwenye kiti.
  8. Matumizi ya Nyama mara kwa mara hata kama ni ya kuchemsha,kukaanga au kuchoma.
  9. Kurithi kutoka kwa wazazi .
  10. Kutojishughulisha na mazoezi.
  11. Maisha ya kuiga kama ulevi wa pombe na kadharika.
DALILI ZA KUA NA KITAMBI AU TUMBO KUBWA 
  1. Tumbo kua kubwa na kubana ukivaa nguo
  2. Uchovu  

TIBA AU NJISI YA KUONDOA KITAMBI/TUMBO KUBWA 
  • Kunywa maji mengi kwa siku walau lita tatu au zaidi na dakika 15 baada ya kumaliza kula au kabla ya kula 
  • Kunywa Green tea kila siku 
  • Kula spicy foods vyakula vyenye viungo
  • Weka nazi katika chakula chako 
  • Tafuna nyanya moja au mbili kila siku 
  • Tangawizi -twanga kipande cha tangawizi kamua maji yake weka na asali kidogo subiri kwa dakika tano na kunywa kila siku .
  • Kunywa juis/maji ya limao kila siku 
  • Tafuna  kitunguu swaumu vipande vitatu au vinne asubuhi  na baada ya hapo kunywa maji ya limao kila siku.
  • Kula mlo mzuri wenye protein matunda na mbogamboga na kuacha vyakula vya waga na junks foods vyakula feki
  • Fanaya mazoezi walau dakika 30 kwa kila siku.
  • Epukana na mawazo.
Kwa ushauri zaidi piga/whatsaap 0718662724.

Thursday, 1 July 2021

JIFUNZE KUHUSU P . I .D/MAAMBUKIZI YA WADUDU KWENYE VIA VYA UZAZI, DALILI ZAKE SABABU NA TIBA PIA


P.I.D/MAAMBUKIZI YA WADUDU KWENYE VIA VYA UZAZI,
P.I.D- Pelvic Inflammatory Disease.
P.I.D Ni maambukizi kwenye via vya uzazi kwa mwanamke ambayo huusisha maambukizi kwenye shingo ya kizazi(CERVICITIS),nyama kwenye mfumo wa wa uzazi(ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi(SALPINGITIS) 
Kuna aina mbili ambayo ni chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa P.I.D ni NEISSERIA GONORNOAE na CHLAMYDIA TRACHOMATIC

WANAMKE ANAUPATAJE UGONJWA WA P.I.D 
-Kupitia ngono zembe
-Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
-Kufanya mapenzi bila kutumia kinga
-Kupitia magonjwa ya zinaa hususani kaswande na kisonono
-Kupitia kunyonywa ukeni mara kwa mara
-Utoaji wa mimba na kutosafishwa vizuri baada ya kutoa mimba
-Kuweka vitu ukeni ili kuufanye uke ubane au kumvutia mpenzi wako
-Kutumia dawa na njia za kuzuia mimba(vijiti na sindano)
- Kuwa na U.T.I. sugu au fungus ya muda mrefu
-Kupitia kufanya mapenzi kinyume na maumbile (haja kubwa)kwa mwanamke.

DALILI ZA P.I.D
-Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri yaweza ukawa njano, mweupe au maziwa
-Uke kutoa harufu mbaya 
-Kuwashwa sehemu za siri
-Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
-Uke kuwa mlaini sana
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa
-Kuvurugika kwa hedhi
-Kutokwa na maji maji ukeni kupita kiasi
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Homa, uchovu na kizunguzungu

MADHARA YA P.I.D 
-Maumivu ya tumbo au nyonga ya mara kwa mara mara baada ya tendo la ndoa. au kipindi cha upevushaji mayai hali hii hutokana na majeraha yaliyopi katika mirija ya uzazi
-Kusababisha majeraha ndani na nje ya mirija za uzazi ambayo hipelekea mirija kuziba
-Kubeba mimba nje ya kizazi husababishwa yai kushindwa kufika kwenywe mji wa uzazi kupitia mirija ya uzazi 
-Ugumba kwa mwanamke
-kupata kansa ya shingo ya uzazi 

JINSI YA KUEPUKANA NA P.I.D
Japo kuwepo na tiba za kujitibu lakini unashauriwa kinga ni bore kuliko tiba hivyo zingatia yafuatayo;-
-Epuka kufanya ngono zembe
-Usifanye mapenzi baada ya kujifungua au mimba kutoka
-Weka tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara
-Kuwa msafi na nguo zako za ndani na kula lishe bora
-Epuka kushare nguo za ndani
-Usifanye mapenzi kinyume na maumbile kupitia haja kubwa,kunyonywa sehemu za siri n.k

UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA HUU WAHI KUPATA MATIBABU. KWANI UGONJWA HUU NI HATARI NA HUWEZA KUKUSABABISHIA UGUMBA AU KANSA YA SHINGO YA KIZAZI

N.B 
Ugonjwa wa P.I.D unatibika vizuri kabisa hivy basi kama upo tayari unaumwa piga namba hii ili kuweza kupata tiba piga/whatsap 0718662724.